Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mradi wa maji Ngudu wakamilika
Habari Mchanganyiko

Mradi wa maji Ngudu wakamilika

Spread the love

SERIKALI imetekeleza mradi wa majisafi kutoka Ziwa Victoria kwenda katika mji wa Ngudu na vijiji vilivyopo kando kando ya bomba linalopeleka maji katika Mji wa Ngudu, anaandika Dany Tibason.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isac Kamwelwe alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki (CCM) ambaye alitaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kuunganisha Mji mdogo wa Malampaka katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ili kuwapatia wananchi maji ya uhakika.

“Serikali imekamilisha mradi wa maji kutika Ziwa Victoria hadi Mji wa Ngudu na vijiji vilivyo karibu na mji huo wilayani Kwimba, mradi huu unatoa maji ya uhakika kuliko miradi ya visima vifupi ambavyo ni vya msimu.

“Lakini Mji mdogo wa Malampaka na vijiji vingine vya karibu na Jihu, Bukigi, Muifa, Kali, Nyababinza na Mwang’horoli ambavyo vipo karibu na Mji wa Ngudu havijaunganishwa kwenye mradi huo.

“Je, serikali haioni umuhimu wa kuunganisha mji mdogo wa Malampaka na vijiji vya Jihu, Bugiki, Muhida, Lali, Nyabanziba na Mwang’horoli katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ili kuwapatia wananchi hao maji ya uhakika?” alihoji Ndaki

Aijibu Mhandisi Kamwelwe amesema mradi huo ilihusisha ulazaji wa bomba la kilomita 25 na sehemu nyingine ya bomba lilitumika bomba la zamani la mradi wa visima uliojengwa miaka ya 70.

Aidha amesema serikali kupitia programu ya maendeleo ya sekta ya maji, imetekeleza miradi ya maji Malampaka, Sayusayu, Mwasayi, Niapanda na Sangamwalugesha ambapo miradi hiyo imekamilika na wananchi wanapata maji.

“Serikali pia imekamilisha usanifu na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwa miradi ya maji ya Mwabulimu, Mwamanenge na Badi ambayo itahudumia vijiji vya Muhida, Jihu na Badi yenyewe, ujenzi wa miradi hii itafanyika katika awamu ya pili ya programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji,” amesema Mhandisi Kamwelwe

Pia amesema serikali imeandaa mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda kwenye miji ya Sumve, Malampaka na Mallya ambapo hadi sasa taratibu za kumpata mtaalam mshauri atakayefanya usanifu wa mradi huo zinaendelea ambapo jumla ya shilingi bilioni mbili zimetengwa katika mwaka wa 2017/18 kwa ajili ya mradi huo ambapo pia utanufaisha baadhi ya vijiji vilivyopo katika Mji mdogo wa Malampaka.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!