Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Biashara Mkurugenzi TPA: Mikataba ya utekelezaji bado haijasainiwa
BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mikataba ya utekelezaji bado haijasainiwa

Spread the love

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema Serikali ya Tanzania bado haijasaini mikataba ya utekelezaji wa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na UAE katika ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo mafunzo, TEHAMA pamoja na uendelezaji na uendeshaji wa bandari (IGA).

Pia amesema Bunge bado halijaridhia mkataba huo wa awali wala TPA haijasaini mkataba na kampuni yoyote kuhusu uendelezaji wa bandarini nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mkurugenzi TPA


Mkataba huo wa awali ulisainiwa tarehe 25 Oktoba 2022  kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Mbossa ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Juni 2023 wakati wa mahojiano yaliyofanyika katika Kituo cha televisheni cha Clouds 360, asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa hoja na elimu kuhusu makubaliano ya mkataba huo kwa Taifa.

Amesema mkataba huo wa IGA pamoja na mambo mengine unaelekeza kwamba kama Serikali ya Tanzania itaridhia ni lazima wakubaliane katika mikataba mingine tofauti na huo wa IGA.

“Kwa sababu kwa kawaida uendeshaji wa bandari haufanywi moja kwa moja na Serikali Kuu yenyewe ila kwetu sisi tumekasimu kwa TPA na wenzetu ni DP World, na ndio maana tunaona kuna kutajwa kwa TPA na DP World.

“Baada ya Bunge kuridhia kutakuwa na mikataba ya utekelezaji wa shughuli husika kwa kuzingatia sheria, kama vile mikataba ya TEHAMA, mafunzo, uendeshaji na uendelezaji ambapo kwa sasa mikataba hiyo bado haijasainiwa,” amesema na kuongeza kuwa;

“TPA haijasaini Mkataba na kampuni yeyote. Mkataba uliosainiwa ni kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano kwenye masuala ya bandari, tehama, mafunzo ya uendelezaji wa bandari, baada ya hapo kutakua na mikataba ya utekelezaji,” amesema.

Kuhusu muda wa mkataba, Mkurugenzi huyo amesema mikataba ya utekelezaji ambayo itaingiwa baada ya mkataba huo wa awali kuridhiwa, itakuwa na muda mahususi.

“Pale muda huu utakapokwisha maana yake na mkataba huu wa awali nao utakuwa umekwisha. Maana yake ni kwamba muda wa mkataba wa awali utaupata katika mikataba hii inayofuatia,” – amesema Mbossa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

NBC kuchochea ustawi biashara kati ya Tanzania na Afrika kusini.

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu dhamira yake...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Biashara

NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1

Spread the loveBENKI ya NMB imezindua rasmi programu mpya yenye hati fungani...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

error: Content is protected !!