Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Biashara Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa
BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the love

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na UAE katika ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo mafunzo, TEHAMA pamoja na uendelezaji na uendeshaji wa bandari (IGA), unaweza kuvunjwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mkataba huo wa awali ulisainiwa tarehe 25 Oktoba 2022 kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ili kuendeleza na kuboresha uendeshaji wa miundombinu ya kimkakati ya bandari za bahari na maziwa makuu, maeneo maalumu ya kiuchumi, maegesho ya utunzaji mizigo na maeneo ya kanda za kibiashara.

Mbossa ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Juni 2023 katika mahojiano yaliyofanyika katika Kituo cha televisheni cha Clouds 360 ikiwa ni mwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa hoja na elimu kuhusu makubaliano ya mkataba huo kwa Taifa.

Amesema katika kipengele cha 23 (3) kinagusia mkataba unaweza kuvunjwa/kusitishwa.

“Pia kinaeleza kuhusu taratibu za kuvunja/kusitisha mkataba na kinaeleza wazi kuwa mwenzako (nchi) haiwezi kukataa “unresoanably”, cha muhimu ni kwamba unaposoma vifungu usome vyote kwa pamoja,” amesema.

Aidha amesema mkataba huu wa awali ukisharidhiwa maana yake kuna taratibu za kisheria inabidi zifuatwe za kuingia mikataba ya utekelezaji ikiwemo majadiliano na kwamba taratibu zote inabidi zifanywe ndani ya miezi 12.

“Kwenye mikataba ya utekelezaji tutajadili “terms” na “consideration” za pande zote mbili lakini pia na suala la muda wa mikataba ya utekelezaji,” amesema.

Aidha, amesisitiza kuwa Serikali ina malengo mazuri ya kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinakua kwa kasi zaidi.

“Lakini pia naishukuru serikali kwa sababu kuna uwazi ambao unaweza tusababishia [hata] tukataa. Si kila nchi inaweza ikaenjoy hiki ambacho tunaenjoy kwamba kuna uwazi kama huu wa kuweza kujua kwamba kuna vitu gani vinaendelea,” amesema.

Amesema Serikali haijasaini mkataba wa miaka 100 wala haijauza  haijaiuza Bandari kwani  ina malengo mazuri na Bandari hiyo.

“Sisi TPA tunahakikisha kwamba tunaendeleza malengo mazuri ya shughuli za bandari kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Na sisi kama TPA tupo committed kuhakikisha kwamba tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kuwapa nafuu Watanzania ambao wanatumia Bandari zetu na nchi nyingine.

“Lakini pia niwaombe tushirikiane katika kuhakikisha tunaendeleza hizi shughuli za Bandari na ziwe na manufaa makubwa kwa uchumi,” amesema Mbossa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

NBC kuchochea ustawi biashara kati ya Tanzania na Afrika kusini.

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu dhamira yake...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Biashara

NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1

Spread the loveBENKI ya NMB imezindua rasmi programu mpya yenye hati fungani...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

error: Content is protected !!