Tuesday , 26 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Mikoa 16 kupata umeme kwa mgawo kuanzia leo
Habari MchanganyikoTangulizi

Mikoa 16 kupata umeme kwa mgawo kuanzia leo

Spread the love

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO)  limetangaza kuzimwa kwa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 Kidatu -Kihansi kwa tarehe 26 hadi 28 Agosti 2023

kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa 12 kamili jioni (01:00 -12:00). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Taarifa iliyotolewa jana Ijumaa na shirika hilo imetaja sababu ya kuzimwa kwa njia hiyo kuwa ni kuruhusu Mkandarasi anayejenga kituo kipya cha kupoza umeme Ifakara kuunganisha kituo hicho kwenye gridi ya Taifa.

Imesema kazi hiyo itahusisha kuunga njia ya msongo wa Kilovoti 220 Kihansi -Kidatu kwenye kituo kipya.

“Kuunganishwa kwa kituo hiki kipya ni muhimu kwani kutasaidia kuongeza ubora na upatikanaji wa umeme katika wilaya za Kilombero, Ulanga na maeneo ya jirani sambamba na kuvutia wawekezaji,” imesema.

Taarifa hiyo imesema, kutokana na kazi hii baadhi ya maeneo kwenye mikoa yataathirika kwa awamu katika nyakati tofauti, ratiba kamili itatolewa kwenye Mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mwanza, Geita na Mara.

“Tutaendelea kuwafahamisha maendeleo ya kazi hiyo hadi kukamilika kwake,” imesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Spread the loveIMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery...

error: Content is protected !!