Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchungaji Kenya ahukumiwa miaka 75 jela
Habari Mchanganyiko

Mchungaji Kenya ahukumiwa miaka 75 jela

Spread the love

ASKOFU katika kaunti ya Kisumu nchini Kenya, Joseph Agutu amehukumiwa kifungo cha miaka 75 jela baada ya mahakama kumkukuta na hatia ya kuwabaka watoto wa kike watatu, huku mmoja kati yao akimuambikiza Virusi vya Ukimwi(VVU). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hukumu hiyo ilitolewa jana tarehe 18 Desemba 2018 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Pauline Mbulika baada ya ushahidi uliotolewa na mmoja kati ya mashahidi katika kesi hiyo, kuthibitisha kwamba askofu huyo alifanya ngono zembe zaidi ya mara tano kwa watoto hao.

Agutu alihukumiwa kifungo hicho na mahakama kutokana na makosa manne yaliyokuwa yakimkabili, ambapo alitenda katika nyakati tofauti kwenye kipindi cha mwezi Aprili na Julai mwaka 2016 katika eneo la Kachok.

Katika makosa hayo, Askofu huyo alishtakiwa kwa kumuambukiza VVU kwa makusudi mtoto mmoja. Agutu amefungwa miaka 20 jela kwa kila kosa katika makosa matatu, wakati kosa la nne akifungwa miaka 15.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!