JITIHADA za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwainua wachimbaji wadogo wa madini, zimeendelea kuonekana baada ya Mchimbaji mdogo wa Dhahabu kutoka Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marwa Maginga kununua mtambo wa uchimbaji wa dhahabu aina ya Katapila kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 200. Anaripoti Paul Kayanda, Mara… (endelea).
Hayo yamebainishwa leo tarehe 4 Septemba, 2022 mkoani Mara katika maonesho ya Mara International Business Expo 2022 yaliyoandaliwa na Chemba ya biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania Mkoa wa Mara.
Maonesho hayo yanalenga kuutangaza mkoa huo kupitia vivutio na fursa kibiashata zilizopo katika eneo hilo kwa Afrika Mashariki.
Akizungumia ununuzi wa mtambo huo, Mchimbaji huyo alisema hatua aliyoipiga inatokana na ari ya Rais Samia kuendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa wachimbaji wadogo.
Alisema Rais Samia amewatengenezea fusa mbalimbali na kwamba kadri siku zinavyozidi kusonga sekta ya uchimbaji mdogo inazidi kuthaminika na wahusika kutumia mwanya huo kuendelea kukuza mitaji yao.
“Sisi wachimbaji wadogo kwa kweli tunaomba Rais wetu mpendwa aendelee kutushika mkono kwa kuendelea kututengenezea mazingira mazuri zaidi ili ifikie wakati nasisi tumudu uchimbaji wa kati na uchimbaji mkubwa,” alisema.
Aidha, Msemaji wa kampuni ya Meta Plant and EQuepment Tanzania Ltd., Edwin Ruangisa ambayo imemuuia mtambo huo alisema; “Kifaa hicho tulichomuuzia mteja wetu kitamsaidia kwa shughuli mbalimbali na siyo uchimbaji wa madini ya dhahabu peke yake, bali kifaa hicho kitamwingizia faida kwa shughuli zingine za ujenzi wa miundo mbinu na majengo.”
Naye Mwenyekiti wa chemba ya biashara mkoa wa Mara, Boniphace Ndengo aliahidi kuendelea kuisaidia serikali kunyanyua uchumi kupitia sekta ya madini kwa kuwashika mkono wachimbaji wadogo.
“Nami nimpongeza Rais Samia kutusaidia sisi wawekezaji wakubwa pamoja na wajasiriamali kupata uthubutu mkubwa kwenda kwenye sekta kubwa kama hizi… hali hiyo inakwenda kujenga ushindani na makampuni makubwa,” alisema Ndengo.
Leave a comment