Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love

MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi ya uzalishaji wahitimu katika taaluma ambazo nafasi za ajira zimepungua ikiwemo walimu, badala yake ielekeze nguvu kwenye kuzalisha wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi, ambao ni rahisi kujiajiri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Shangazi ametoa maoni hayo leo tarehe 22 Aprili 2024, bungeni jijini Dodoma, akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha wa 2024/25, iliyowasilishwa na waziri wake, Prof. Kitila Mkumbo.

Mbunge huyo wa CCM amesema sera ya elimu inapaswa kufanyiwa marekebisho ili iwe na mikakati ya kuzalisha watanzania ambao watakuja kuwa wazalishaji wazuri wa Taifa.

“Jambo mahususi nilitaka nishauri, bado tunazalisha sana watumishi katika kada ya walimu ambayo haiwezi kuajiri, vijana wengi wako mtaani hawajaajiriwa lakini bado vyuo vyetu vinaendelea kuzalisha walimu. Tunaomba wizara ilitizame hili jambo kwa upana kwamba kuna vyuo 35 vya Serikali vinazalisha walimu, je tuna umuhimu wa kuendelea kuwazalisha,” amesema Shangazi na kuongeza:

“Nadhani vizuri mipango ikatuelekeza tuwe na wanafunzi wengi kwenye vyuo vya aina ya DIT,  huku tuwe na wanafunzi wengi ambao hata baadae hawatatusumbua kulazimika kuwatafutia ajira sababu watajiajiri wenyewe kulingana na maarifa watakayopata kupitia vyuo hivi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

error: Content is protected !!