Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the love

WIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake ya kiasi cha Sh. 121.3 bilioni, katika mwaka ujao wa fedha wa 2024/25. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa 2024/25, yamewasilishwa leo tarehe 22 Aprili 2024, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.

Prof. Mkumbo amesema Sh. 100.2 bilioni zimetengwa  kutumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. 21.8 zikipangwa kutumika katika miradi ya maendeleo.

Waziri huyo wa uwekezaji ametaja vipaumbele vitakayofanyiwa kazi 2024/25, ikiwemo ufufuaji mradi mkubwa wa eneo la kiuchumi la Bagamoyo, unaojumuisha ujenzi wa bandari mpya na ukanda maalum wa viwanda.

Prof. Mkumbo amesema katika mwaka ujao wa fedha wamepanga kutangaza mradi wa Bagamoyo kwa wawekezaji wa nje ya nchi,  kwa nia ya kuendeleza mradi kwa njia mbalimbali, ikiwemo ubia na sekta binafsi kwa kufuata mpango uliorejewa.

“Tumepanga kufanya uendelezaji wa miradi ya kitaifa ya kielelezo,  ikiwa nipamoja na kuanza hatua za awali za kuandaa mipango kabambe, upembuzi yakinifu, kufanya uthamini katika maeneo maalum ya uwekezaji ambayo hayakuthaminiwa awali na kufanya malipo ya fidia ya maeneo ya Bagamoyo, Tanga na Manyoni,” amesema Prof. Mkumbo.

Mkataba wa kuanza utekelezaji mradi huo ikiwemo ujenzi wa  bandari ya kisasa ya Bagamoyo ulisainiwa Oktoba 2015 katika Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais mstaafu Jakata Kikwete, ambapo awamu ya kwanza ya utekelezaji wake ilitakiwa ikamilike 2017. Hata hivyo, mradi huo ulifutwa 2018 kwenye Serikali ya Hayati Dk. John Pombe Magufuli.

Mnamo Septemba 2023, Prof, Mkumbo alipokea taarifa ya upembuzi yakinifu na mpango wa ujenzi wa mradi huo, ambapo alisema utagharimu Sh. 11 trilioni ambapo utatumia hekta 9,800.

Mbali na ufufuaji mradi wa Bagamoyo, Prof. Mkumbo ametaja vipaumbele vingine vya wizara yake kwa 2924/25, ikiwemo kukamilisha uandaaji wa sera mpya ya uwekezaji na mkakati wake wa utekelezaji, kukamilisha uunganishaji wa kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)na mamlaka ya maeneo ya uzalishaji wa mauzo ya nje (EPZA).

Vingine ni kuanzisha taasisi mpya ya kusimamia masuala ya uwekezaji wa sekta binafsi, kukamilisha mwongozo wa ujenzi na uendeshaji wa kongani wa viwanda nchini.Kuendelea kusimamia utekelezaji wa mageuzi katika uendeshaji wa mashirika ya umma, ikiwemo kuendelea kubaini mashirika ambayo majukumu yake yamepitwa na wakati au yanaingiliana na majukumu ya taasisi zingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!