Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge asema utawala wa sheria ndiyo kivutio uwekezaji, biashara
Habari za Siasa

Mbunge asema utawala wa sheria ndiyo kivutio uwekezaji, biashara

Mbunge wa Madaba, Joseph Mhagama
Spread the love

 

MBUNGE wa Madaba, Joseph Mhagama, amesema kivutio namba moja cha wawekezaji na biashara nchini ni utawala wa sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mhagama ameyasema hayo bungeni leo Alhamisi tarehe 28, Aprili wakati akichangia hoja makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara wa Sheria na Katiba kwa mwaka 2022/23.

Amesema kama hakuna utawala wa sheria hatutaweza kuvutia uwekezaji na kusisitiza kuwa wawekezaji hawawekezi penye utawala wa uongozi bali pale penye utawala wa sheria.

“Hapa ni kazo juu ya uatawala wa shjeria dhifi ya utawala wa viongozi tumepiga hatua kubwa awamu hadi awamu tumetoka kwenye uatawala wa uongozi kwenda utawala wa sheria”

Amesema katika awamu ya sita Serikali imefanya mabadiliko makubwa ya kutoka kwenye utawala wa viongozi kwenda kwenye utawala wa sheria.

Mbunge huiyo amesema katika mwaka huu watanzania milioni moja na nusu wamepata elimu juu ya utawala wa sheria katika Wiki ya Sheria.

Amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana bado kuna changamoto ya kuwafikia wananchi huko chini ikiwemo Madaba.

Alisema watu wengi wanaoendesha kesi huko chini hawana weledi akitolea mfano wa jeshi la polisi kuwa na mamlaka ya kukamata, kufanya upelelezi na kushtaki. “haki itapatikanaje kwenye mazingira haya”

Amesema ili kuondokana na changamoto hizo lazima ofisi ya mwendesha mashataka aongezewe fedha ili aweze kuwafikia watu wengi.

Amesema hadi Februari mwaka huu kesi za jinai 42,132 zimefunguliwa kupitia Ofisi ya Mwendasha Mashtaka lakini ni asilimia 28 tu ya kesi zilizopatiwa ufumbuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!