October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe avamiwa

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, yupo kwenye wakati mgumu jimboni kwake Hai, Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro…(endelea).

Akiwa kwenye mkutano jana tarehe 3 Machi 2020, alivamiwa na vijana walioandaliwa kuvuruga mkutano wake, ikiwa ni hatua za kuzima kile kilichoitwa dhamira ya kugombea tena ubunge kwenye jimbo hilo.

Mkutano huo ulikuwa ukifanyika katika Kijiji cha Kikafu Chini, Kata ya Weruweru, ambapo kikundi cha vijana wa kike na kiume liliibuka na kuanza kufanya vurugu.

Akiwa jukwaani anahutubia, ziliibuka kelele za vijana hao na kusababisha kunyamaza kwa muda, vijana hao walimshambulia Mbowe kwa maneno ikiwa ni pamoja na kusema ‘tunamtaka Magufuli.”

Polisi waliokuwepo eneo la tukio, waliomba msaada na baadaye polisi wengine waliongezwa ili kukabili uvamizi wa vijana hao kwenye mkutano huo. Hata hivyo, polisi hawakukamata mtu hata mmoja licha ya kuonekana waziwazi.

error: Content is protected !!