October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mauaji afisa mtendaji Dar, watatu mbaroni

Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam

Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya afisa mtemtendaji wa serikali ya mtaa wa Mbezi Msumi Kelvin Costa Mowo (38), Mkazi wa Bunju. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari leo Jumnne tarehe 12 Oktoba 2021 amesema, “majina ya watuhumiwa hao yanahifadhiwa kwa saababu za kiupelelezi.”

Amesema, tukio hili limetokea jana Jumatatu saa 11:54 asubuhi eneo la Msumi Mbezi wilaya ya Ubungo katika ofisi za Serikali ya mtaa, ambapo marehemu akiwa ofisini kwake anasikiliza mgogoro wa ardhi.

“Ghafla watu wapatao wanne waliingia ofisini na mmoja wao akatoa panga na kumshambulia mtendaji huyo kitendo kilichopelekea kupata majeraha makubwa na baadae akapoteza maisha wakati akikimbizwa hospitalini.”

“Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo wanahojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo,” amesema Kamanda Muliro

error: Content is protected !!