Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko DAWASA yawalipa mamilioni wananchi, RC Makalla awapongeza
Habari Mchanganyiko

DAWASA yawalipa mamilioni wananchi, RC Makalla awapongeza

Spread the love

 

MRADI wa maji wa mshikamano, Jimbo la Kibamba, umeanza kushika kasi baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kuwalipa mamilioni ya fedha wakazi wanaopisha ujenzi wa mradi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni mradi wenye thamani ya Sh.5.4 bilioni unaotekelezwa kati ya DAWASA na Kampuni ya Advent Construction Limited, ukitekelezwa kwa miezi 12 kuanzia tarehe 15 Oktoba 2021. Mkataba wa utekeleza umekwisha kusainiwa chini ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Leo Jumanne, tarehe 12 Oktoba 2021, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla ameshiriki shughuli ya kukabidhi fidia wananchi hao jumla ya Sh.236.6 milioni kwa kila moja na kiwango chake kwa wananchi wanaopisha mradi huo.

Shughuli hiyo, imefanyikia Bohari Kuu ya DAWASA, Boko jijini humo ambapo RC Makalla alianza kwa kukagua vifaa mbalimbali mabomba makubwa na madogo yatakavyotumika kwenye mradi huo na maeneo mengine ikiwamo Mwabepande, Chanika na mengine hususan ya pembezoni.

“Leo ni mara ya pili nakuja hapa, nilikuja hapa nikiwa naibu waziri wa maji na hapa ndipo panaitwa bohari na hapakuwa hivi. Ilikuwa ni bohari isiyokuwa na kitu ila leo ni bohari iliyosheheni vifaa mbalimbali. Nikupongeze sana CEO (Cyprian Luhemeja) kwa haya, kwani yanatoa matumaini kuwa mmejipanga kutoa huduma na uwezo mnao,” amesema Makalla

Amesema, eneo hilo lilikuwa linatumika kwa watumishi waliokosea kwenye wizara au serikalini “njia ya kukukomoa ilikuwa unaletwa huku, unakutana na mabomba yaliyooza, mijusi lakini leo mnaonesha mko tayari kutekeleza maagizo ya Rais wetu mpendwa, Mama Samia.”

“Nimefurahi namna ambavyo DAWASA mmekuwa wepesi sana wa kushughulikia kero na kuwa karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa, mimi nimewapima taasisi katika ziara ya kutatua kero za wananchi jimbo kwa jimbo, hakuna sehemu DAWASA mmekosa, mnaonesha mko tayari kuwahudumia wananchi,” amesema

Mkuu huyo wa mkoa, amewashukuru wananchi hao waliotoa maeneo yao ili mradi huo uweze kutekelezwa na kuwaomba wanancho wengine kutoa ushirikiano kwa DAWASA ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa na kumalizika kwa wakati.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema, miongoni mwa maelekezo waliyopewa ni kuhakikisha wanapeleka huduma ya maji maeneo ya pembezoni na tayari wameanza kufanyia kazi ikiwemo Jimbo la Kibamba.

“Kwa sasa, tunahakikisha tunakuwa na mabomba ya kutosha ya ukubwa mbalimbali, vifaa ili kumaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa maji,” alisema

Aidha, Mhandisi Luhemeja alimweleza RC Makalla kwamba mchakato wa kuwa na “gharama moja kwa wateja wote wa majumbani ya kuwaunganishia imekwisha kufanyiwa kazi na tumeiwasilisha kwa bodi ili wakiidhinisha tutaitangaza kwa wananchi.

Maeneo yatakayonufaika na mradi huo utakapokamilika ni, Mpiji, Mshikamano, Magohe, Msakuzi Kaskazini, Machimbo, Majengo Mapya, Dodoma, Luguruni Lapaz, Mbezi Inn, Magari saba, Magayana na Njia Panda Makondeni.

Mengine ni, Kwa gamba, Takukuru, Luguruni Dampo, Luguruni KKKT, Rising Star, Msakuzi Supermarket, Aman Street, Miti Mirefu, Madafu, Kwa mfala, Chikongwe, Masaki Street, Mbezi Msumi, Machimbo na Mageti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

error: Content is protected !!