July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mastaa wawili Yanga warejea kambini 

Spread the love

 

WACHEZAJI Haruna Niyonzima pamoja na Lamine Moro wamerejea kwenye kambi ya klabu hiyo, Kigamboni Jijini Dar es Salaam mara baada ya kusimamishwa kwa muda na  kutokana na utovu wa nidhamu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wawili hao wamerejea mara baada ya kuonekana kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na wadhamini wa klabu hiyo, kampuni ya Gsm, kwenye kambi ya Yanga iliyoko kwenye mji wa Avic, Kigamboni, mara baada ya kutoonekana eneo hilo kwa muda mrefu.

Niyonzima na Lamine wamerejea kikosini wakati timu hiyo ikifanya maandalizi ya kukamilisha michezo yao miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Ihefu na Dodoma Jiji kabla ya kwenda kuvaana na Simba kwenye fainali ya kombe la Shirikisho itakayopigwa Kigoma, tarehe 25 Julai 2021.

Haruna Niyonzima

Kwa upande wa Haruna Niyonzima alitimuliwa na kocha Nabi siku chache kabla ya mchezo dhidi ya Simba mabo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Zawadi Mauya dakika ya 12.

Kwa upande wa nahodha wakikosi hiko Lamine Moro yeye alikuwa nje ya kikosi hiko, kwa miezi miwili mara baada ya kutozuka kwa sintofahamu kati yake na kocha Nabi.

Lamine Moro, nahodha wa Yanga

Lamine alirudishwa Dar es Salaam, kutokea Ruangwa mkoani Lindi, wakati wa kikosi hiko kikiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC.

Kwa Habari zaidi soma Gazeti la Raia Mwema leo

 

error: Content is protected !!