Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki 10,000 kuingia uwanjani kwenye mchezo wa kufuzu fainali kombe la Dunia kesho kati ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Benin. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Mchezo huo wa kundi J, utapigwa kesho Alhamisi Oktoba 7, 2021 majiora ya saa 10 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Akizungumza kuelekea mchezo huo Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’ Clifford Ndimbo amesema kuwa Caf wameruhusu idadi ya mashabiki 10,000 kutazama mchezo huo.
“Tumepokea taarifa ya kuruhusiwa mashabiki 10,000 kushuhudia mchezo wa kesho na tayari tumeshaweka viingilio rafiki kuhakikisha watu wanajitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao.” Alisema Ndimbo
Taifa Stars inaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa vinara kwenye kundi J, wakiwa na pointi nne mara baada ya kucheza michezo miwili.
Akitaja Viingilio hivyo Afisa Habari huyo alisema kuwa kiingilio cha chini kitakuwa shilingi 3000 kwa kuwa kitakuwa rahisi kwa kila mtu.
“Viingilio vilivyowekwa ni 5000 kwa VIP B na C na shilingi 3000 kwa mzunguko, utaona kiingilio ambacho kila mmoja anaweza kukimudu na tujitokeze Uwanjani kesho”.
Mara baada ya mchezo Star itasafiri usiku kuelekea nchini Benin kwa ajili ya mchezo wa marudiano kundi J, utakaopigwa Oktoba 10, 2021
Leave a comment