Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Mamba wanatafuna watu Mto Rufiji’
Habari Mchanganyiko

‘Mamba wanatafuna watu Mto Rufiji’

Spread the love
MOHAMMED Mchengelwa, Mbunge wa Rufiji amesema, changamoto ya uhaba wa maji inahatarisha maisha ya wananchi wake, kufuatia baadhi yao kuliwa na mamba wanakichota maji katika Mto Rufiji. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mchengelwa ameyasema hayo leo tarehe 24 Juni 2019 bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu.

Amesema, tatizo la uhaba wa maji katika jimbo lake ni kubwa, hali inayopelekea wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo, huku wengine wakithubutu kuchota maji katika mto rufiji ambao una mamba wengi.

Kufuatia changamoto hiyo, Mchengelwa ameihoji serikali ina mpango gani wa kuiondoa changamoto hiyo.

“Tatizo la maji kwenye Wilaya ya Rufji ni kubwa sana,  hali iliyopelekea nguvu kubwa ya vijana na kina mama kupotea wakijaribu kutembeea umbali  mrefu na kudiriki kuchota maji mto rufiji. Na kupeleka wananchi wengi kuchukuliwa na mamba,” amesema Mchengelwa na kuongeza;

“Serikali ina mpango gani wa kuja kufanya tathimini ikizingatiwa kwamba Rufiji ni kanda maalum na pia tunatekeleza mradi wa kufua umeme wa stiegler’s Gorge,  lini itakuja kufanya tathimini ya tatizo la maji . Wananchi wanatumia km 7 mpaka kumi kutafuta maji, lini serikali itachimba visima virefu ili kuwaondolea adha wananchi.”

Akijibu swali hilo, Jumaa Aweso, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji amesema serikali inatambua changamoto hiyo na kwamba imefanya jitihada mbalimbali katika kukabiliana nayo ikiwemo kujenga visima virefu 13 katika jimbo hilo.

Aweso amesema baada ya ujenzi wa visima kukamilika, serikali itafanya usanifu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji.

“Tunatambua maji ni uhai na ni moja ya changamoto kubwa, tumefanya jitihada kubwa ya kuchimba visima 13 pale vyenye thamani ya zaidi milioni  400. Tumeshachimba 10 , baada ya ukamilikishaji wa visima tutafanya usanifu katika kuhakikisha tunafanya miradi mikubwa ili wananchi wako wapate maji, “ amesema Aweso.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!