Monday , 5 June 2023
Home Kitengo Michezo Mahakama yampa onyo kali Wema
Michezo

Mahakama yampa onyo kali Wema

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imerejesha dhamana ya Wema Sepetu, Msanii wa Filamu nchini huku ikimpa onyo la kutorejea kukiuka masharti ya dhamana. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Wema alifutiwa dhamana yake tarehe 11 Juni 2019 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Maira Kasonde baada ya kukiuka masharti yake.

Kwenye kesi hiyo, upande wa serikali unawakilishwa na Wakili Jenifer Masue, huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Albert Msando na Ruben Simwenzi.

Baada ya kukaa kwa wiki moja mahabusu, leo terehe 24 Juni 2019, mahakama hiyo imeamua kurejesha dhamana yake ambayo ilizuiwa kutokana na Wema kushindwa kuhudhuria kwenye kesi hiyo hapo awali.

Msanii huyo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, anakabiliwa na tuhumza za kuchapisha picha za uchi kwenye mtandao na kisha kusambaza.

“Mahakama inakuonya, pale haupo mahakamani kwasababu yoyote ile ijulishe mahakama, mshitakiwa anapokuwa nje kwa dhamana, anakuwa chini ya ulinzi wa mdhamini.

“Endapo akishindwa mdhamini, ataondolewa na mahakama itamfutia dhamana mshtakiwa…kwa sasa tunakupa onyo na dhamana yako itaendelea,” amesema Hakimu Kasonde. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 4 Julai mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Yanga waitwa Ikulu kesho Jumatatu

Spread the love RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu, tarehe...

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

error: Content is protected !!