Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majimbo manne yafutwa Z’bar
Habari za Siasa

Majimbo manne yafutwa Z’bar

Jaji Mkuu Mstaafu, Hamid Mahmoud Hamid, Mwenyekiti wa ZEC
Spread the love

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imefuta majimbo mane ya uchaguzi visiwani Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Jaji Mkuu Mstaafu, Hamid Mahmoud Hamid, Mwenyekiti wa ZEC ametangaza uamuzi huo leo tarehe Alhamisi tarehe 2 Julai 2020.

Baada ya mabadiliko hayo, kwa sasa Zanzibar ina majimbo 50 badala ya 54 ilivyokuwa awali, ambapo Unguja ina majimbo 32 na Pemba 18.

Jaala Makame, Afisa Habari wa ZEC, akizungumza na MwanaHALISI ONLINE kwa simu, amesema majimbo manne yaliyofuta yanatoka upande wa Unguja.

Makame amesema, mabadiliko hayo hayajagusa upande wa Pemba. Hata hivyo, hakuwa tayari kueleza sababu za kupunguzwa kwa majimbo hayo.

“Ni sahihi, majimbo manne ya Unguja yamepunguzwa, upande wa Pemba hakuna mabadiliko yoyote,” amesema Makame.

Mabadiliko hayo yamekuja mwezi mmoja baada ya Chama cha ACT-Wazalendo, kulalalamika kwamba ZEC ina mpango wa kupunguza majimbo visiwani humo.

Malalamiko hayo yalitolewa tarehe 30 Mei 2020 na Nassor  Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar, siku kadhaa baada ya ZEC kuanzisha mchakato wa upokeaji maoni ya vyama vya siasa na wananchi kuhusu kupitia upya mipaka ya majimbo ya uchaguzi Zanzibar.

Katika taarifa yake hiyo, Mazrui alisema chama chake hakiungi mkono zoezi la ukataji upya wa majimbo kwa madai kwamba ni kinyume cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inayotaka majimbo yakatwe kila baada ya miaka 8 hadi 10.

Mazrui alisema mara ya mwisho ZEC ilikata majimbo mwaka 2015, hivyo miaka 8 bado haijafika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!