Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Majangili yatelekeza porini nyara za serikali
Habari Mchanganyiko

Majangili yatelekeza porini nyara za serikali

Meno ya tembo
Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mbeya kwa kushirikiana  na askari wa TANAPA wamekamata pikipiki sita  zikiwa zimepakia nyara za serikali katika pori la hifadhi ya Taifa la Ruaha liliopo katika kijiji cha  Nyamlala  tarafa ya Rujewa wilayani Mbarali, anaandika Mwandishi Wetu.

Nyara zilizokamatwa ni pamoja na ngozi moja ya simba na vipande 15 vya meno ya tembo vikiwa vimepakiwa katika pikipiki hizo huku zikiwa zimetekelezwa na wahusika ambao walikimbia.

Tukio hilo limetokea baada ya kuwapo msako mkali wa  jeshi la polisi na askari wa TANAPA katika hifadhi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya , Mohammed Mpinga amesema baada ya pikipiki hizo kukamatwa wahusika walikimbia na kuzitekeleza katika pori hilo.

Kamanda Mpinga amesema kati ya pikipiki hizo, mbili zilikuwa hazina namba za usajili huku nyingine zikiwa ni  MC 386 BHW aina ya Kinglion, MC T.799 CTW aina ya T-Better, MC 755 ADJ, T.461 BZE.

Aidha, Mpinga amesema pikipiki hizo baada ya kukaguliwa zilikutwa na nyara za serikali ambazo ni ngozi moja ya Simba na vipande 15 vya meno ya Tembo.

“ Upelelezi na ufuatiliaji unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wa tukio hili ili waweze kuchukukuliwa hatua zinazostahili”amesema  Kamanda Mpinga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!