Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mahakama yanusuru afya ya Seth wa IPTL
Habari Mchanganyiko

Mahakama yanusuru afya ya Seth wa IPTL

James Rugemarila na Harbinde Seth (kulia)
Spread the love

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeliamuru Jeshi la Magereza na Mamlaka zinazohusika na mshtakiwa wa IPTL,   Harbinder  Seth  kumpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu, anaandika Mwandishi Wetu.

Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa huyo kuomba nafasi ya kujieleza kuhusu hali yake.

Aidha, mahakama hiyo iliagiza mamlaka zinazohusika na mshtakiwa huyo kuwasilisha taarifa ya mshtakiwa huyo kupata huduma za matatibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

“Suala la mshtakiwa ni la msingi na ni haki yake kupata huduma hiyo mara ya mwisho mahakama yangu ilitoa amri kwamba mshtakiwa apelekwe hospitali ya Muhimbili, lakini imepuuzwa… tarehe inayokuja mahakama hii inataka taarifa za mshtakiwa huyo kuhakikisha amepata huduma inayostahili” amesema

Awali kabla ya kutolewa amri hiyo, Sethi alidai kuwa hali yake kiafya bado ni mbaya na kwamba alitolewa gereza la Segerea na kupelekwa hospitali ya Amana, lakini hakupata huduma inayostahili kwa sababu maradhi yake yanahitaji daktari na  mtaalamu.

“Mheshimiwa hali yangu ni mbaya sana nilipelekwa hospitali ya Amana, lakini sikupata huduma kutokana na maradhi yangu kuhitaji daktari mtaalamu… ” alidai Sethi wakati akiomba mahakama kwenda kutibiwa.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali , Vital Peter alidai suala la ugonjwa ni la kitaalamu ambalo linahitaji kuthibitishwa ili kujiridhisha na kwamba mshtakiwa hajawasilisha nyaraka zinazounga mkono kutoka kwa mtaalamu kuelezea hali yake.

Alidai kutibiwa ni haki ya mshtakiwa kwa kuwa wapo wataalamu katika hospitali  ya Muhimbili na magereza.

Hata hivyo, alidai upelelezi wa shairi hilo haujakamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itatajwa  Agosti 3, mwaka huu pamoja na kuangalia hatma ya upelelezi.

Mbali na Seth, mshtakiwa mwingine ni James Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa VIP Engineering na mmiliki mwenza wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), ambao wanakabiliwa na mashitaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani  milioni 22. 1 na Sh bilioni 309 pamoja na utakatishaji fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

error: Content is protected !!