Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa: 28 Oktoba siyo siku ya mzaha
Habari za Siasa

Majaliwa: 28 Oktoba siyo siku ya mzaha

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kampeni za CCM wilayani Monduli
Spread the love

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amemaliza ziara yake mkoa wa Mara na kuwaeleza wananchi Jumatano tarehe 28 Oktoba, 2020 siyo siku ya mzaha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

“Tarehe 28 Oktoba, 2020 siyo siyo ya mzaha na wala siyo siku ya majaribio. Ni siku ya kuchagua kiongozi atakayetufaa na huyo si mwingine bali Dk. John Pombe Magufuli,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana Jumanne tarehe 22 Septemba 2020 wakati akizungumza na wakazi wa Kibara, wilayani Bunda, mkoani Mara kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea wa CCM uliofanyika katika uwanja wa michezo wa Kibara.

Amesema kiongozi wa nchi anayefaa kuchaguliwa ni yule anayeweza kusimamia rasilmali za Taifa.

“Ni yule anayeweza kusimamia tunu za Taifa, siyo mnapata kiongozi halafu akipewa nchi anabadilisha hadi wimbo wa Taifa.”

“Tunahitaji kiongozi anayeweza kupambana na rushwa, awe mtu wa kutetea watu wake wapate haki bila kuombwa rushwa. Huyo si mwingine bali ni Dk. John Pombe Magufuli,” amesema.

Majaliwa ambaye alikuwa mkoani Mara kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli alitumia fursa hiyo kuwaombea kura mgombea ubunge wa jimbo la Mwibara, Charles Kajege na diwani wa Kibara, Nyanguli Mtesigwa na madiwani wengine wa jimbo hilo. Jioni hii anaingia mkoa wa Mwanza.

Akielezea umuhimu wa chama kuwa na Ilani ya Uchaguzi, Majaliwa amesema Chama cha Mapinduzi kimeandaa ilani yake yenye kurasa 303 ikisimamia yale yaliyokuwemo kwenye ilani iliyopita ambayo ilikuwa na kurasa 236 na mengine mengi mapya.

“Watekelezaji wa hayo yote yaliyoainishwa kwenye Ilani ni hawa watatu ambao nawaombea kura leo. Namwombea kura Dk. Magufuli ili akamilishe aliyoyaanza na atekeleze yaliyomo kwenye Ilani ya sasa. Ni lazima tumpatie mbunge na diwani wa CCM ili waweze kuzungumza lugha moja.”

Kuhusu uboreshaji kwenye sekta ya afya, Mheshimiwa Majaliwa alisema zilitumika sh. bilioni 1.8 za kujenga hospitali ya wilaya hiyo na bado kuna sh. milioni 152 zilitolewa ili kuisaidia Halmashauri kujenga zahanati.

Kuhusu sekta ya maji, Majaliwa amesema Sh.6.2 bilioni zimetumika kukarabati na ujenzi wa miradi mbalimbali kwenye Halmashauri ya wilayani Bunda, ikiwemo uchimbaji wa visima virefu na vifupi, utengenezaji wa matenki ya kuvuna maji na uchimbaji wa mabwawa.

“Vijiji vilivyonufaika na miradi hii ni Nyatwali, Nyamuswa, Mgeta –Nyang’aranga, kinyabwiga, Bulamba na Kibara. Pia jumla ya Sh.90.1 milioni zimetumika kwa ajili ya ukarabati na usafishaji wa pampu za mkono 67 na visima vitatu,” amesema.

Mapema asubuhi, akiwa kata ya Kisorya, Majaliwa aliwaeleza wananchi hao kwamba Serikali ya CCM ina mpango wa kuboresha kituo chao cha afya kwa kuongeza wodi tatu za wanawake, wanaume na watoto.

Pia alisema zimetengwa Sh.550 milioni za kuimarisha kituo hicho kwa kuongeza majengo ya jiko, chumba cha kufulia na chumba cha kuhifadhia maiti.

Kuhusu barabara, amesema kiasi cha Sh.2.9 bilioni kimetumika kutengeneza barabara za kuunganisha vijiji kwa vijiji, kukarabati sehemu korofi zilizoharibiwa na mafuriko, madaraja, makalvati na matengenezo ya kawaida.

Kuhusu umeme, amesema vijiji 77 kati ya 78 vina umeme isipokuwa kijiji kimoja tu cha Nafubu kilichopo kisiwani, ambacho amesema watapelekewa huduma ya umeme wa jua kwa vile siyo rahisi kupitisha nyaya za umeme majini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!