Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif amwita Lissu ampe mbinu za ushindi
Habari za Siasa

Maalim Seif amwita Lissu ampe mbinu za ushindi

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo anataka kukutana na Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema ili ampe mikakati ya ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Unguja … (endelea).

Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti chama hicho ametoa kauli hiyo jana Jumanne tarehe 22 Septemba 2020 katika mkutano wake na timu za ushindi za mikoa na majimbo ACT-Wazaendo za Unguja.

Alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka mikakati yake ya kumtafutia ushindi Rais John Pombe Magufuli, Mgombea wake Urais wa Tanzania na kwamba Lissu anatakiwa awe na mbinu za kupangua mikakati hiyo.

“Kule bara kuna mikakati yao yote nimeshaambiwa na mimi nataka nikutane na Lissu nimpe mikakati hiyo na nimwambie akiweza kuzuia mikakati hiyo wamekwisha hawa,” alisema Maalim Seif.

Tundu Lissu, Mgombea Urais Tanzania (Chadema).

Kuhusu uchaguzi huo, Maalim Seif aliswma mpinzani wake wa karibu Dk. Hussein Ali Mwinyi, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM anapaswa kujiandaa kushindwa huku akimtaka Dk. Magufuli kukusanya virago vyake kwa maelezo kwamba hawatashinda katika Uchaguzi Mkuu huo.

“Mara hii rafiki yangu Magufuli ajiandae kufunga Virago vyake na Hussein Mwinyi akikubali ajiandae kua Makamu wangu wa Kwanza wa Rais. Mara hii kichwa lazima kitoke ACT-Wazalendo,” alisema Maalim Seif.

Hivi karibuni, Lissu akiwa Zanzibar alitangaza kumuunga mkono Maalim Seif kwenye mbio za urais huku Maalim Seif naye ameweka wazi kumuunga mkono Lissu.

Chadema imesimamisha mgombea urais wa Zanzibar, Said Issan Mohamed ambaye Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemteua kugombea urais.

Pia, ACT-Wazalendo imemsimamisha Bernard Membe, kugombea urais wa Tanzania na tayari amekwisha zindua kampeni zake za urais mkoani Lindi ingawa kwa sasa haendelei na kampeni.

Jana Jumanne, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akihutubia mkutano wa kampeni wa mgombea Ubunge wa Tabora Mjini kupitia chama hicho, Msafiri Mtemelwa alisema, mazungumzo ya kushirikiana yamekamilika.

Zitto alisema, mazungumzo ya kusimamisha mgombea mmoja wa nafasi ya urais, kuachiana majimbo na kata nayo yamenalizika na tarehe 3 Oktoba 2020 katika mkutano wa kampeni

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!