MSITU wa Chato mkoani Geita, kama ambavyo umekuwa ukitambulishwa toka awali, sasa utaitwa Msitu wa Silayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).
Silayo ni jina la, Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za
Misitu (TFS), Prof. Dos Santos Silayo ambaye ndiye aliyesimamia uanzishwaji wa shamba hilo la misitu.
“Badala ya kuita Shamba la Miti Chato, sasa litaitwa Shamba la Mti Silayo. Watanzania wajue kama mtu akifanya kazi nzuri, basi atakumbukwa kwa kazi nzuri,” amesema
“…kwa kazi nzuri ya kamishna iliyofanywa na vijana hawa walioandaa shamba hili. Shamba hili linastahili kuitwa Prof. Silayo Forest kuanzia leo,” amesema Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa shamba hilo leo Jumatano tarehe 27 Januari 2021, lililopo eneo la Butengo, Chato mkoani Geita.
Kwenye uzinduizi huo, Rais Magufuli amesema, ni vizuri sasa badala ya vitu kuvipa majina ya wanasiasa, sasa tuyape majina ya watu waliofanya kazi vizuri na kwamba, wakumbukwe kwa kazi zao nzuri.
Kiongozi huyo wa nchi amesema, Prof. Silayo amefanya kazi kubwa ya shamba hilo ambalo litaiingizia nchi fedha nyingi.

Rais John Magufuli kutangaza rasmi Shamba la Miti la Chato liitwe Shamba la Silayo.
Pia, Rais Magufuli amempa Kamishna Silayo kuongeza nguvu katika suala la usafirishaji magogo kwa kuwa, kufanya hivyo kunapeleka kazi nje ya nchi na kulitia hasara taifa.
“Kamishna hili suala la kusafirisha magogo uweke nguvu za kutosha. Najua kusafirisha magogo nje sio tu inatukosesha mapato, bali tunawakosesha wananchi wetu fursa za ajira. Unaposafirisha magogo nje, unakuwa umesafirisha ajira nje,” amesema na kuongeza:
“Ni vema basi tujipange katika siku za usoni kuhakikisha hizi mali, ikiwemo misitu yetu inatumika hapa hapa kutengeneza vifaa vinavyotokana na misitu ili nchi iweze kupata fedha nyingi zaidi.”
Amesema, mpaka sasa shamba hilo lenye ukubwa wa ekari elfu 69 limetoa ajira kwa zaidi ya watu 800.
Leave a comment