May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbatia: Tuchukue tahadhari ya corona

Spread the love

 

JAMES Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha siasa cha upinzani nchini Tanzania cha NCCR-Mageuzi, ameshauri wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Kelvin Mwaipugu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbatia amesema hayo leo Jumatano tarehe 27 Januari 2021, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya NCCR-Mageuzi, Ilala jijini Dar es Salaam.

“Taarifa za kidunia zinaonyesha, virusi vipya vya ugonjwa huu wa corona kutoka Afrika Kusini, Brazil na Ulaya vipo na maambukizi yake yameongezeka kutoka asilimia 30 mpaka 70, hivyo hatuna budi kujingika kwa kila Mtanzania,” amesema Mbatia

“Ni wajibu wetu sote kulinda uhai wetu kwa gharama yoyote kwa kuwa ni janga la kidunia, tuondoke gizani kwa kila mtu kuchukua tahadhari kwa kuwa kila mtu ana haki ya kuishi. Watanzania tusiulize Mama Tanzania anatufanyia nini bali tujiulize tunamfanyia nini Mama Tanzania katika janga hili,” amesema

Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), amesema “suala la uhai ni jambo la mtu binafsi, hatuhitaji kibari cha Serikali katika kujilinda kwenye jambo hili, naomba Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake tuchukue tahadhari kujikinga na janga hili

Mbuge huyo wa zamani wa Vunjo Mkoa wa Kilimanjaro amesema “vyombo mbalimbali vitoe taarifa sahihi na serikali yetu ishirikiane na mashirika mbalimbali kwa ajili ya thamani ya uhai wa maisha ya binadamu kwa sababu haki ya kuishi haupewi na binadamu.”

Tunaungana na waraka wa Baraza la Maskofu uliotoka jana juu ya kuchukua taadhari kwa janga hili na tunaishauri Serikali kuungana na jumuiya ya kimataifa katika kupambana na janga hili, kwani Tanzania haiwezi kuwa kisiwa katika janga hili.

Jana Jumanne tarehe 26 Januari 2021, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Gervas Nyaisonga aliwaandikia barua Mwadhama, Mpelekwa wa Baba Mtakatifu, Maaskofu Wakuu, Maaskofu na Maaskofu Wastaafu akiwataka kuchukua tahadhari ya maambukizi mapya ya corona.

Nyaisonga ambaye ni Jimbo Kuu anasema, kuna wimbi jipya la maambukizo ya corona kufuatia nchi kadhaa kuthibitisha kupita kwenye kipindi kigumu cha kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo.

Amesema “hatuna budi kujihami, kuchukua tahadhari na kumlilia Mungu kwa nguvu zaidi, ili janga hili lisitukumbe.”

Rais wa TEC, anazidi kueleza maaskofu wenzake, kwamba “kwa uhalisia huo, tusiache kuwashauri, kuwahimiza na kuwaongoza Taifa la Mungu katika mapambano haya dhidi ya virusi vya Korona.”

error: Content is protected !!