Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Corona: JPM ‘hatutegemei kujifungia’
Habari za SiasaTangulizi

Corona: JPM ‘hatutegemei kujifungia’

Rais John Magufuli
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amesema, hana mpango wa kuifungia nchi (lock down), kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato … (endelea).

Akizungumza kwenye uzinduzi wa shamba la miti Chato, mkoani Geita leo Jumatano tarehe 27 Januari 2021, Rais Magufuli amesema, Watanzania waendelee kuchukua tahadhari na wasitishwe.

“Katika kipindi hiki magonjwa yanayojitokezatokeza yasiyojulikana kama corona, nchi nyingi wananchi wake watakuwa wamejifungia ndani. Sisi Watanzania hatujajifungia ndani na hatutegemei kujifungia ndani.

“…na wala sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani, kwa sababu Mungu wetu yuko hai na ataendelea kutulinda Watanzania,” amesema Rais Magufuli.

Akizungumza kwenye hadhara hio iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi, kiongozi huyo wa nchi amesema, tahadhari ambazo Mtanzania anapaswa kuzichukua ni pamoja na kujifukiza pia kuswali.

“Umajifukizia huku unamuomba Mungu, unaswali, unasali huku unapiga zoezi la kufanya kazi ya kulima mahindi ili ule vizuri, ushibe corona ishwinde kuingia kwenye mwili wako.

“Mtatishwa sana, ndugu zangu Watanzania lakini simameni imara. Ninajua wapo baadhi ya Watanzania hata wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine kwenda kuchanjwa, walipochanjwa huku walikuja kutuletea corona ambayo ni ya ajabu ajabu, simameni imara,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, kama Wazungu wangekuwa na uwezo wa kuleta chanjo, basi chanzo za magonjwa mengine kama kansa, kifua kikuu na malaria wangekuwa wamishazipata.

“Chanjo hazifai, kama wazungu wangekuwa wana uwezo wa kuleta chanzo, hata chanjo ya UKIWMI ingekuwa imeishaletwa, hata chanjo ya kifua kikuu… kifua kikuu kingekuwa kimeisha ondoka, hata chanzo ya maleria ingekuwa imesihapatikana, hata chanjo ya kansa ingekuwa imeishapatikana,” amesema.

Amewataka Watanzania kuwa waangalifu kwa kile alichoitwa ‘mambo ya kuletewa letewa,” na kwamba, Wtatanzania wasifikirie wanapendwa sana na mataifa ya nje.

“Na niiombe Wizara ya Afya isiwe inakimbilia machanjo chanjo bila yenyewe kujiridhisha. Ipo nchi fulani walichanjwa watoto wake wa kike wenye umri wa miaka 14, wanaambiwa ni kwa ajili ya kuzuia kansa ya kizazi, imekuja kugundulika ile chanjo ni ya kuwazuia wasizae.

“Niwaombe sana Wizara ya Afya, sio kila chanjo ni ya maana sana kwa taifa letu, sio kila chanjo ina faida kwetu, ni lazima Watanzania tuwe macho. Ni lazima Watanzania tuwe waangalifu. tutafanyiwa majaribio ya ajabu ambayo yataleta madhara makubwa,” ametahadharisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!