May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maelfu wapata chanjo ya corona Dar, siku zaongezwa

Spread the love

ZAIDI ya wananchi 2,882 mkoani Dar es Salaam, leo Jumapili tarehe 22 Agosti 2021, wamepata chanjo ya ugonjwa wa corona (UVIKO-19), katika Uwanja wa Uhuru, mkoani humo.Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, wakati zoezi hilo likiendelea uwanjani hapo.

“Hadi saa 4.00 asubuhi tayari wananchi 2,882 walikuwa wamepokea chanjo. Kila aliyepokea chanjo amepatiwa cheti kinachotambulika kimataifa,” amesema Makalla.

Kufuatia mwitikio huo mkubwa wa wananchi kupata chanjo, Makalla ameongezea muda ambapo zoezi hilo lililoendeshwa na watumishi wa afya zaidi ya 100, litaendelea hadi kesho Jumatatu.

Makalla amewaomba wananchi kutumia fursa hiyo ili wapate chanjo kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo.

error: Content is protected !!