May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Manny Pacquiao adundwa, ahamishia nguvu urais

Spread the love

Bondia mkongwe Manny Pacquiao (42) mapema alfajiri ya leo, amekutana na wakati mgumu baada ya kupoteza pambano lake la kuwania ubingwa wa dunia dhidi ya Yordenis Ugas.

Yordenis raia wa Cuba, licha ya kwamba hakuwa mlengwa namba moja wa pambano hilo bali alingia kama mbadala wa Errol Spence Jr aliyeumia siku chache kabla ya pambano hilo, ameshinda kwa ushindi wa pointi za majaji wote watatu ‘Unanimous Decision’.

Pambano hilo lililopigwa katika huko Las Vegas nchini Marekani, limemwezesha Yordenis Ugas kuwa mshindi rasmi taji la ubingwa la WBA uzani wa Super Welter.

Aidha, baada ya kumaliza pambano hilo, Pacquiao ambaye ni seneta huko nchini Ufilipino, amesema pambano hilo lilikuwa kama bonus kwenye masisha yake ya ndondi na sasa anaelekeza nguvu zake kutumia wafilipino.

Mshindi huyo mara nane wa dunia, anatajwa kujipanga kuwania urais mwaka kesho kumrithi rais wa sasa Rodrigo Duterte.

error: Content is protected !!