Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Michezo Madrid, PSG vitani UEFA leo
Michezo

Madrid, PSG vitani UEFA leo

Spread the love

 

HATUA ya 16 ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya itaendelea hii leo kwa kupigwa michezo miwili, ambapo Real Madrid itakuwa ugenini kuvaana na PSG ya nchini Ufaransa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mchezo huo wa mtoano utapigwa majira ya saa 5 usiku kwenye dimba la Parc De Princes nchini Ufaransa.

Tukio la kuvutia kwenye mchezo huo ni kumshuhudia Sergio Ramos akishuka dimbani kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani aliyoitumikia katika kipindi cha miaka 16 akiwa kama nahodha.

Mchezaji huyo aliondoka ndani ya Madrid kwenye dirisha kubwa la usajili, na kujiunga na matajiri hao wa jijini Paris kwa uhamisho huru.

Kabla ya mchezo huu wa leo Real Madrid na PSG wamekutana mara sita, kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na Madrid wamefanikiwa kuondoka na ushindi kwenye michezo mitatu na kwenda sare mara mbili, huku PSG akiibuka na ushindi kwenye michezo mmoja tu.

Kwenye michezo hiyo, Real Madrid wamefanikiwa kupachika jumla ya mabao nane kwenye michezo yote sita, tofauti ya bao moja kwa PSG ambao wamefunga mabao saba.

Mchezo mwengine hii leo utapigwa kwenye dimba la Jose Alvalade nchini Ureno, ambapo Sporting Lisbon itashuka dimbani dhidi ya Manchester City na nchini England.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!