Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Machifu wajinasibu kufanya kazi kwa ukaribu na makanisa, serikali
Habari Mchanganyiko

Machifu wajinasibu kufanya kazi kwa ukaribu na makanisa, serikali

Spread the love

UMOJA wa Machifu wa Chigogo katika Mkoa wa Dodoma umesema kuwa umejipanga kufanya  kazi kwa ukaribu na mashirika ya dini pamoja na serikali kwa kuwa kazi zao zinafanana kwa lengo kubwa la kukemea maovu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Hayo yalielezwa na Chifu wa Chigogo, Pemba Yadunda alipokuwa akitoa salamu katika kanisa la Covenant Fact Church (Baba wa Matendo Pentecoste lenye makao makuu yake Njedengwa Kata ya Dodoma Makulu Jijini Dodoma.

Akitoa salama katika ibada maalumu ya kuliombea taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu, Baraza la Mawaziri, Bunge na Mahakama alisema kuwa umoja huo umekuwa ukifanya kazi ya kukemea maovu pamoja na kujenga misingi bora inayozuia masuala mazima ya unyanyasaji na ukandamizaji.

Ibada hiyo iliyoambatana na mkutano wa hadhara lengo kubwa ikiwa ni kupeleka ukombozi wa Kimungu kwa taifa na jamii kwa ujumla wake, mmoja huyo wa machifu alisema kuwa kwa sasa umefika wakati wa kupambana na mila potofu inayoambatana na unyanyasaji.

“Sisi machifu tunafanya kazi kwa ukaribu zaidi na taasisi za dini na Serikali, kwa kuwa Serikali inakemea maovu na kanisa linakemea maovu na machifu tunakemea maovu kwa nguvu zetu zote sambamba na kupiga vita vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

“Tunakubaliana na baadhi ya mila ambazo hazina madhara ambazo zinaendana na utamaduni wa Kitanzania na Kiafrika lakini tunapinga kwa nguvu kubwa mila na destuli ambazo zinalenga kumtharirisha mtanzania ikiwa ni pamoja na kuiga tabia mbovu za Kimagharibi,” alisema Chifu Yadunda.

Kwa Upande wake Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Damasi Slivester akimkaribisha muhubiri katika ibada hiyo alisema kuwa kanisa  linafanya kazi na jamii ya watu ambao lengo lao ni kuhakikisha wanakemea maovu ambayo ni chukizo mbele za Mungu.

“Leo katika hii ibada nimeona umuhimu wa kuwakaribisha hawa machifu kwa kuzingatia umuhimu wao katika jamii kwa kuwa ni sehemu ya kuzuia matendo maovu na kwa umuhimu huo ni lazima wakawa sehemu ya jamii ya watu ambao wana kiu ya kwenda mbinguni.

“Kanisa lazima litambue kuwa linafanya kazi kwa ukaribu na serikali kwa kufuata sheria za nchi pamoja na taratibu zake lakini na serikali inafanya kazi kwa ukaribu na kanisa kwa kutambua huduma inazofanya kwa kuhakikisha kanisa linasaidia kukemea na kuzuia maovu kwa maana ya kuwahubiria watu kuacha dhambi na kutenda matendo mema” alisema Askofu mkuu wa Kanisa hilo Damasi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!