Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif ‘akusanya’ kijiji Pemba
Habari za Siasa

Maalim Seif ‘akusanya’ kijiji Pemba

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, amekusanya wananchi wa Pemba na kusikiliza kero zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pemba … (endelea).

Badala ya kupanda jukwaani na kuhutubia, akiwa Chakechake Pemba, Maalim Seif leo Jumanne tarehe 13 Oktoba 2020 ameshiriki mazoezi na timu za Wete na Gado.

Baada ya kumaliza mazoezi, alikaa kwenye kiti chake pamoja na wanachama wengine huku kundi kubwa la wananchi wakiwa pamoja naye kila mmoja akipata nafasi ya kuzungumza jambo lake.

Kwenye mazungumza hao, Maalim Seif alitoa fursa pana kwa vijana ambao walieleza mambo kadhaa yanayowakwaza hususani ukosefu wa ajili.

Kiongozi huyo nguli wa siasa za upinzani Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho, amewaleza vijana hao dhamira yake ya kugombea urais kuwa ni kuifanya Zanzibar ijiamulie mustakabali wake.

Kwenye staili hiyo mpya ya kampeni zake, Maalim Seif alikuwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa chama hicho huku akisema “wakati ni sasa.”

Maalim Seif amerejea kauli yake kwamba, msimamo wake aliokuwa nao wakati akiwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), haujayumba.

Na kwamba, Zanzibar yenye mamlaka kamili ndio msimamo ataoendelea nao hata baada ya kuwa rais wa visiwa hivyo iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

“Dhamira yangu ni Zanzibar yenye mamlaka kamili. tutajiamulia kuhusu kilimo na wapi tuuze, tutafanya yale tunayohitaji kama nchi,” amesema.

Amewataka Wazanzibar kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na wamchague ili dhamira hiyo aioneshe kwa vitendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!