November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea: Hii ndiyo kazi ya kwanza nitaifanya bungeni

Spread the love

MGOMBEA Ubunge wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo, Saed Kubenea amesema, akishinda ubunge kipaumbele chake cha kwanza ni kuhakikisha waliovunjiwa nyumba zao mabondenu wanalipwa fidia. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Kubenea ameyasema hayo jana Jumatatu tarehe 12 Oktoba 2020 katika mkutano wake wa kampeni alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kata ya Kigogo ambayo ni miongoni mwa waliokumbwa na adha ya kuvunjiwa nyumba zao.

“Siendi bungeni kujifunza, nafahamu kila kitu bungeni, mimi nikiingia ajenda yangu ya kwanza ni mabondeni, wananchi wangu waliobomolewa nyumba zao walipwe fidia na wapewe maeneo mapya yenye huduma za jamii sio kuwachukua watu kuwapekeka ambapo hakuna huduma” alisema.

Kubenea alisema, ana uzoefu na nafasi hiyo kwa kuwa amekuwa mbunge kwa miaka mitano kati ya mwkaa 2015-2020 jimbo la Ubungo na anazijua shida za wananchi wa Kinondoni.

“Nimekuwa mbunge kwa miaka mitano, nimekuwa mwandishi wa habari za bunge kwa miaka 17 na nimekuwa Mtanzania ninayetetea haki za watu ambaye ni kimbilio la wanyonge, mnyonge mwenzenu ni mimi nitawatumikia” amesema.

“Jimbo la Kinondoni kuna wagombea wengi, msiharibu kura zenu kwa kupeleka kwa kila mtu, ili tumshinde Abbas Tarimba (mgombea wa CCM) kura zenu nipeni mimi” amesema.

error: Content is protected !!