Wednesday , 22 May 2024
Home Habari Mchanganyiko M23 wauteka mji muhimu DR Congo
Habari Mchanganyiko

M23 wauteka mji muhimu DR Congo

Spread the love

WAASI wa M23 wamedai kuuteka mji muhimu wa Kitshanga/Kitchanga katika eneo la Masisi nchini DR Congo baada ya siku tatu za mapigano. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Mashirika ya kiraia na majeshi ya Umoja wa Mataifa nchini DRC yamelaani mashambulizi hayo ya kijeshi ya M23, ambayo sasa yamesukuma zaidi ya raia 400,000 kuyakimbia makazi yao. Redio ya Okapi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti kuanguka kwa Kitshanga kwa waasi.

Picha za mamia ya watu waliokimbia mji huo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii. “Ndiyo… sasa tuna Kitshanga na vitongoji vyake”, msemaji wa M23, Willy Ngoma aliambia BBC jana tarehe 27 Januari 2023.

Wakati wa kuanguka kwa Kitchanga, seneta wa DRC Francine Muyumba alitoa wito kwa bunge kuitisha kikao cha dharura kwa sababu nchi ifikia pabaya.

Mchakato wa amani wa Luanda uliomba M23 kusitisha mapigano na kujiondoa katika maeneo ambayo imeteka, lakini waasi, wengi wao wakiwa wa kabila la Kitutsi, wanasema wanalazimika kuingilia kati kukomesha mauaji mengine ya kimbari yasitokee dhidi ya Watutsi.

Kitshanga ni mji muhimu ulio katika njia ya mwisho iliyo wazi kati ya vitovu vikuu vya kiuchumi vya Kivu Kaskazini vya Goma na Butembo.

Kwa miaka kadhaa, Kitshanga imekuwa ngome na makao makuu ya kiongozi wa waasi maarufu Laurent Nkunda na kundi lake la waasi la CNDP, ambalo baadaye lilikuja kuwa M23.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the love  Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya...

Habari Mchanganyiko

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk....

error: Content is protected !!