JESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia kupatikana kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Jovine Clinton, anayedaiwa kupotea tangu tarehe 24 Jnauari 2023, akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Wito huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe 28 Januari 2023 na Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye, akizungumza na MwanaHALISI Online.
Simbeye amedai kuwa, mara ya mwisho alionana na Clinton tarehe 24 Januari mwaka huu, katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, wakisikiliza Kesi Na. 570/2023 iliyofunguliwa na wajumbe wa zamani wa Bodi ya Wadhamini ya NCCR-Mageuzi, wakipinga uteuzi wa wajumbe wapya.
“Hadi sasa hatujui yuko wapi, anafanya nini na anaishije leo ni siku ya nne, tarehe 24 tulikuwa naye katika kesi mahakamani alikuwa anaongoza wenzake katika timu ya vijana alishinda hadi saa 12.00 jioni. Aliporudi nyumbani kwake majira ya saa 4.00 alitoka nje ya nyumbani kwake kwa ajili ya kupunga upepo ndipo alipopotea,” amedai simbeye na kuongeza:
“Niombe Jeshi la Polisi kutumia vyombo vyake mbalimbali vya kiuchunguzi na ufuatiliaji ili kuhakikisha kijana mwenzetu anapatikana sababu kazi yake ni kulinda raia na mali zake.”
Leave a comment