Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Likizo ya mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT yawa gumzo
Habari MchanganyikoTangulizi

Likizo ya mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT yawa gumzo

Mch. Dk. Eliona Kimaro
Spread the love

 

TAARIFA ya likizo ya siku 60 ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dk. Eliona Kimaro, zilizoanza kuenea katika mitandao ya kijamii na zimezua hisia tofauti miongoni mwa waumini na wasio waumini wa kanisa hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi,” amesema Askofu Mkuu Emmaus Mwamakula, Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki.

Gumzo limeenea katika mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa video inayomwonesha Kimaro akiwaaga waumini wake kwa kile alichoeleza ni kupewa likizo ya siku 60 baada ya kikao na wakuu wa jimbo.

Kimaro amesema katika video hiyo kuwa majukumu yake yatafanywa na Mchungaji Anna na kueleza kuwa barua hiyo ya likizo imemwelekza kuripoti makao makuu ya Dayosisi tarehe 17 Machi mwaka huu.

“Imenilazimu kutii na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti katika ofisi ya askofu kama nilivyoelekezwa na ofisi ya askofu,” amesema Mch. Kimaro.

Katika andiko lake Askofu Mwamakula amesema huenda misimamo binafsi ya Mch. Kimaro ndiyo imemuweka katika misukosuko.

“Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani,” amesema.

Kusimamishwa kwa Mch. Kimaro kumeibua wanasiasa na wanaharakati wengi kueleza hisia zao juu ya hatua hiyo ambapo aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob ameandika katika ukurasa wake wa twitter, “binafsi sishangai kabisaaa kuona maelfu ya Watu wameguswa kuhusu sakata la Mch.Kimaro,

Mchungaji Kimaro amekuwa Msaada kwa Watu na familia nyingi sana KIMARO unamwambia “biashara zangu haziendi vizuri”akwambii tupige magotini tusali,bali mnaanza Kijadili ‘Principles’ za biashara.”

Naye James Mbowe ameandika, “hii taarifa imenistua sana usiku huu, mimi ni mlutheri nitaandika maoni yangu kesho, akili ikitulia.

Duru zinaeleza kuwa huenda kusimamishwa kwa Mch. Kimaro kuna husiana na kauli zake ambazo zimekuwa na utata.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu kama vijana wa Kiislamu pia amewahi kusikika katika video moja akisifu Kanisa Katoliki dhidi ya makanisa mengine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!