May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ligi Kuu Bara kuendelea leo, michezo miwili kupigwa

Mbeya City

Spread the love

 

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea tena leo, ambapo michezo miwili itapigwa kwenye viwanja tofauti. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ligi hiyo ilisimama kwa ajili ya kupisha michezo ya kimataifa iliyokuwa kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) pamoja na maombolezo kufuatia kifo cha Hayati John Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayati Magufuli alifariki tarehe 17 Machi, 2021, kwenye hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam na TFF kutoa agizo la kusimamisha michezo kwa siku 21 kupisha maombolezo ya msiba huo.

Michezo itakayopigwa leo itawakutanisha Mbeya City ambao watakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya wataikabili Kagera Sugar, huku Namungo wataawalika Ihefu FC.

Ligi hiyo inaendelea kwa mzunguko wa 23 kwa baadhi ya timu itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo mitatu.

Mpaka Ligi hiyo inasimama Yanga ilikuwa juu kwenye msimamo ikiwa na pointi 50 ikiwa imecheza michezo 23, ikifuatiwa na Simba kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 huku ikiwa imecheza michezo 20.

error: Content is protected !!