WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema kuwa kuteuliwa kwake kuwa waziri wa wizara hiyo pamoja na uteuzi wa Makamu wa Rais, Dk. Philipo Mpango kunaonesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaimani kubwa na wana Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mwigulu ameyasema hayo hii leo tarehe 8 Machi, 2021, Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha mpango wa tatu wa maendeleo.

Katika maneno yake ya ufunguzi wakati wa hotuba hiyo, Mwigulu ambaye ni shabiki wa klabu ya Yanga alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteuwa kwenye nafasi hiyo pamoja na kumteua Dk. Philip Mpango na hivyo kuonesha imani kubwa kwa mashabiki hao wa Yanga.
“Mheshimiwa Spika kwa kipekee napenda kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kuniteuwa kuwa Waziri wa Fedha, kwa uteuzi wangu na uteuzi wa Makamu wa Rais, Dk. Mpango inaonesha rais anaimani kubwa na wana Yanga,” alisema.

Mwigulu aliteuliwa tarehe 31 Machi, 2021 na Rais Samia kuwa Waziri wa Fedha na Mipango akitokea Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa hafla ya kumuapisha Makamu wa Rais, Dk. Mpango.
Leave a comment