May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Hoseah anavyojipanga kuongoza TLS, atoa ushauri Takukuru, DPP

Dk. Edward Hoseah, mgombea Urais TLS

Spread the love

 

TAREHE 15 Aprili 2021, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kitafanya uchaguzi mkuu wa viongozi mbalimbali ikiwemo urais, watakaoongoza chama hicho kwa mwaka mmoja. Anaripoti Matrida Peter…(endelea).

Wanachama watano wamejitosa kuwania nafasi hiyo ya urais ambao ni; Albert Msando, Francis Stolla, Flaviana Charles, Shehzada Walli na Dk. Edward Hoseah.

MwanaHALISI TV limefanya mahojiano maalum na Dk. Hoseah, aliyewahi kuhudumu nafasi mbalimbali ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuanzia mwaka 1995 hadi 2015, ikiwemo ya mkurugenzi mkuu.

Katika mahojiano hayo, Dk. Hoseah amezungumzia masuala mbalimbali, kama vile kilichomsukuma kuwania nafasi hiyo, anachotaka kukifanya TLS, anavyojitofautisha na wagombea wenzake.

Dk. Hoseah, anavyotizama suala la haki, uadilifu na utu, nini Takukuru wanapaswa kukifanya ili kuwa na kesi zenye mashiko na ushahidi wenye tija bila kuwaweka watuhumiwa mahabusu kwa muda mrefu, ushauri wake kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Anazungumzia jinsi misimamo yake hususan kusimamia kanuni, unavyowashinda baadgi ya watu.

error: Content is protected !!