Spread the love

 

HATIMA ya Mwimbaji nguli wa mtindo wa Rumba wa kutoka Jamhuri ya Kidemorkasia ya Kongo (DRC), Koffi Olomidé inatarajiwa kufahamika leo tarehe 13 Disemba, 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Leo alasiri ndio siku ambayo Mahakama ya Rufaa ya mjini Versailles nchini Ufaransa itatoa uamuzi wake katika kesi ya mashtaka ya unyanyasaji wa kingono yanayomkabili Koffi

Upande wa mashtaka uliomba, Oktoba mwaka jana, kifungo cha miaka nane jela dhidi ya msanii huyo

Bado haihafahamika iwapo Koffi Olomide atakuwepo mahakamani kujua hatima yake au lah!

Mawakili wake wanasema kuwa mteja wao hana hatia na wana imani kwamba atafutiwa mashtaka.

Aliposikilizwa, mwezi Oktoba mwaka huu, Koffi Olomidé alikosoa mashataka hayo aliyoyaita kuwa ni ya uongo kutoka upande wa mashitaka.

“Hizi ni tuhuma zisizokuwa na msingi… ni njama za kutaka kuharibu kazi yangu,” alisema.

Mwimbaji huyo alikuwa akijibu shutuma za wanawake wanne kutoka DRC, kati ya wacheza densi wake wa zamani ambao waliwasilisha malalamiko kati ya mwaka 2007 na 2013.

KOFFI OLOMIDE

Wanamtuhumu kwa kuwafungia kwenye banda lenye ulinzi karibu na jiji la Paris, wakati wa alipokuwa akitembelea Ufaransa na kuwalazimisha kufanya naye mapenzi, bila ridhaa yao. Koffi Olomidé alijitetea na kukanusha tuhuma zote.

Akiwa na umri wa miaka 65, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kujieleza hadharani kuhusu mashtaka dhidi yake.

Hata hivyo, hakuhudhuria kesi yake ya kwanza mwaka 2019 mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Nanterre nchini Ufaransa, ambapo alikuwa amehukumiwa katika mahakama ya mwanzo kifungo cha miaka miwili jela.

Katika mahakama hiyo Koffi alihukumiwa kwa unyanyasaji wa kingono kwa mmoja wa wasichana hao aliyechukuliwa kuwa alikuwa umri ambao haumruhusu kufanya mapenzi.

Hata hivyo Koffi aliachiwa baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha lakini baadaye alifunguliwa mashtaka mengine.

Mwendesha mashtaka wa umma, ambaye alihitaji kifungo cha miaka saba, alikata rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *