January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dewji akoleza moto ujenzi uwanja wa Simba, atoa Bil 2

Mohammed Dewji ‘Mo’

Spread the love

 

RAIS wa heshima wa Simba ya jijini Dar es Salaam, Mohamed Dewji ameiomba bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo, kukutana ili kuandaa utaratibu wa haraka wa ujenzi wa uwanja wao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwekezaji huyo ndani ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho ameanza kwa kuchangia Sh.2 bilioni.

Dewji amesema hayo leo Jumatatu, tarehe 13 Desemba 2021, kupitia akaunti yake ya Twitter akizungumzia safari hiyo ya kuanza mchakato wa ujenzi wa uwanja.

“Nimepokea maoni mengi ya WanaSimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo. Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili.”

“Naomba Bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji. Kwa Kuanza naahidi kuchangia Tsh. 2 billioni. Nawaomba wanasimba tuchange sote,” ameandika Dewji

error: Content is protected !!