February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba ang’aka Uwanja Mkwakwani

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba

Spread the love

KOCHA Mkuu wa Simba, Patric Aussems ameonekana kutorizishwa na nyasi za uwanja wa Mkwakwani uliopo mkoani Tanga mara baada ya kufanya mazoezi ya siku mbili na kikosi chake ambacho kitaivaa JKT Tanzania  ambao watakuwa wenyeji wachezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Aussems amebainisha hayo kupitia ukurasa wake unaopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter mara baada tu yakuwasili na kikosi chake mkoani humo kwa ajili ya kusaka alama tatu ambazo zitamsaidia katika kutetea ubingwa wa ligi hiyo.

“Hali ya Uwanja Tanga kwa mchezo wetu wa kesho dhidi ya JKT, kivipi inawezekana? Maendeleo ya mpira katika nchi yatawezekana kama kutakuwa na miundombinu mizuri.”

Simba ambao toka ligi ianze msimu huu wamekuwa hawana rekodi nzuri wanapokuwa katika michezo ya ugenini, katika michezo mitatu Simba iliyocheza ugenini imefanikiwa kushinda mmoja, sare mmoja na kupoteza mmoja dhidi ya Mbao FC katika Uwanja wa CCM Kirumba.

error: Content is protected !!