Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la Balozi Jumiya ya Ulaya, utata mtupu
Habari za SiasaTangulizi

Sakata la Balozi Jumiya ya Ulaya, utata mtupu

Spread the love

UTATA umeibuka juu ya hatima ya baadaye ya Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini Tanzania, Roeland Van De Geer. Anaaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wakati taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikisema, Serikali ya Jamhuri imemfukuza nchini Balozi Roeland Van na kumuaru kuondoka haraka iwezekano, kuna taarifa nyingine zinasema, balozi huyo hajafukuzwa na serikali. 

Taarifa inayodaiwa kutolewa na msemaji wa ubalozi wa EU jijini Dar es Salaam inasema, taarifa zinazodai kuwa Balozi Roeland Van amefukuzwa nchini hazina ukweli.

“Ukweli ni kwamba, Balozi Roeland Van ameitwa Makao Makuu (Brussels), nchini Ubelgiji, kwa ajili ya kushauriana juu ya siasa na uhusiano wa baadaye kati ya Jumuiya ya Ulaya na Tanzania,” imeeleza taarifa kupitia mitandao ya kijamii, inayodaiwa kutolewa na msemaji wa ubalozi huo.

Hata hivyo, taarifa inayodaiwa kutolewa na msemaji wa ubalozi haina jina la mtoaji wala anuani ya mahali ilikotolewa.

Aidha, taarifa kuwa Balozi Roeland Van ameitwa makao makuu kwa ajili ya kinachoitwa, “kuangaliwa upya uhusiano wa kati ya serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya,” haikueleza kwa undani sababu za kuitwa huko.

Vilevile, hata taarifa inayodaiwa kuwa ya serikali inayoeleza ya kufukuzwa kwa balozi huyo nchini, haikueleza sababu za  kuchukua hatua hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Balozi Roeland Van anatakiwa kuondoka nchini kabla ya saa sita usiku wa tarehe 3 Novemba.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na waliobobea kwenye nyanja ya diplomasia ya kiuchumi wanasema, taarifa zote mbili – kufukuzwa ama kuitwa makao makuu kwa balozi – hazina afya njema kwa taifa.

“Hata kama ameitwa makao makuu, bado hiyo habari njema kwa Tanzania,” anaeleza Dk. Marccossy Albenia, mtafiti na mchambuzi wa masuala ya uchumi wa diplomasia.

Anasema, “ikiwa Ulaya wameona kuna mahusiano mabaya na Tanzania na hivyo wamemuondoa balozi wao nchini na kumtaka atoe maelezo ya hali halisi na akapate maelezo upya, hii ni hatua mbaya zaidi, kuliko kumfukuza.”

Anasema, “ni sharti serikali itafakari haraka mahusiano yake kidiplomasia. Siyo sifa kuwa mgomvi, ndio maana kuwa diplomasia, kwamba utatua changamoto zako kwa njia ya kujenga mahusiano mema.”

Naye mmoja wa aliyepata kuwa balozi wa Tanzania katika nchi za Ulaya, Marekani na Umoja wa Mataifa na ambaye baadaye akaja kuwa waziri katika serikali ya Benjamin Mkapa anasema, “..kama madai haya ni ya kweli, tunakoelekea kutakuwa ni kubaya sana.”

Mwanadiplomasia huyo mashuri nchini anasema, muda siyo mrefu taifa litashuhudia Brussels ikitoa kauli kupitia Bunge lao. Tunachukua mkondo mbaya sana utakaoweza kutusababishia matatizo makubwa ya kiuchumi na kisiasa huko mbele.”

Kutikisika kwa uhusiano kati ya EU na Tanzania, kutaweza kuyumbisha kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi, ikiwamo mchango katika sekta ya elimu, afya na maji.

Kwa mujibu wa mwenendo wa bajeti kuu ya serikali, nchi 14 wanachama wa jumuiya ya Ulaya, ndio wachangiaji wakubwa wa bajeti ya serikali.

Jumuiya ya Ulaya, ni muungano wa nchi 28 ikiwamo Uingereza, ambayo miaka miwili iliyopita, Waziri Mkuu, Theresa May, alitangaza kuiondoa  katika Muungano unaounda umoja huo.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza mkutano muhimu wa viongozi wa umoja huo, huko Brussels, Ubelgiji, kujadili mpango wa Uingereza wa kujiondoa EU, May alisema, kikwazo kilichobaki  sasa kati ya EU na Uingereza, ni suala la mpaka wa Ireland ambao ingependa kubaki katika umoja huo.

Mapema jana viongozi wa EU walipendekeza muda zaidi wa miezi 21 hadi 2021 ili kuruhusu mazungumzo zaidi ya mahusiano ya kibaiashara.

May aliwahikishia viongozi wenzake wa EU kuwa hakutakuwa na mgogoro wowote wa mpaka baina ya Ireland  na Ireland ya Kaskazini. Aliomba kuongozewa muda wa kipindi cha mpito hadi Desemba 2020.

Mbali na Uingereza, wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya, ambao wanawakilishwa na Balozi, Realand Van nchini, ni pamoja na Austaria, Belgium, Bulgaria, Croatia na Jamhuri ya Cypurus.

Wengine, ni Czech, Denmark, Estonia, Finland, France, Ujerumani, Greece, Hungary, Ireland na Italy.

Wapo pia Latvia, Lithuania, Luxembourg, Malta, Netherlands, Poland, Portugal, Romania, Slovakia, Spain, Sweden na Uingereza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!