March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba achukizwa na kambi Zanzibar

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba

Spread the love

KOCHA mkuu wa klabu ya Simba Patrick Aussems ameonekana kutovutiwa na maandalizi ya timu yake visiwani Zanzibar katika kuelekea mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria utakao chezwa 12 january, 2019 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kitu kikubwa ambacho hakijamvutia kocha huo ni sehemu ya malazi kwa timu yake pamoja na miundombinu ya kufanyia mazoezi hayajamridhisha ikiwa kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa klabu bingwa siku ya Jumamosi.

Kocha huyo ameeleza hisia zake hizo kupitia kurasa zake za kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na Instagram ikiwa timu hiyo ina siku ya nne tu toka itue visiwani humo.

“Tumepokelewa vizuri hapa Zanzibar, watu wenye upendo wa kweli lakini kwa bahati mbaya malazi na miundombinu kwa ajiri ya mazoezi havistahili kwa klabu ambayo inajiandaa kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa.”

Si mara ya kwanza kocha huyo kulalamikia swala la miundombinu ya kimichezo hasa viwanja katika nchi hii, ikumbukwe katika mchezo wa Simba waliocheza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoni Tanga kocha huyo alitoa malalamiko yake juu ya ubovu wa uwanja huo.

Simba iliwasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya kucheza michuano ya Kombe la Mapinduzi huku wakati huo huo wakitumia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi ya michezo yao ya hatua ya makundi kwenye Kombe la Klabu Bingwa.

error: Content is protected !!