Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Hospitali ya Mkapa kufanya upasuaji wa tezi dume kisasa
Afya

Hospitali ya Mkapa kufanya upasuaji wa tezi dume kisasa

Hospitali na Benjamini Mkapa ya Dodoma
Spread the love

KWA kipindi ya miezi nane yaani Machi hadi Desemba mwaka jana Hospitali ya Benjamini Mkapa imewatibia wagonjwa 187 wa tezi dume. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na daktari bingwa wa upasuaji wa magojwa ya njia ya mkojo Dk. Remigius Rugakingira alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya utoaji wa matibabu ya tezi dume.

Dk. Rugakingira alisema kuwa hospitali ya Benjamini Mkapa kwa sasa inauwezo wa kutibu tezi dume kwa kutumia njia za kisasa ambapo wafanafanya upasuaji wa ndani kwa ndani na upasuaji wa matundu ambapo alisema utaalamu huo umekuwa mzuri kwa wagonjwa.

Alisema upasuaji wa ndani kwa ndani pamoja na upasuaji wa matundu unamwezesha mgonjwa kupona haraka bila kutumia muda mrefu huku akisema mgonjwa huyo hawi na kidonda kama ilivyokuwa ikitumika zamani.

Akitoa ufafanuzi Dk. Rugakingira alisema kuwa wagonjwa wa tezi dume wanaotibiwa katika hospitali ya Benjamini Mkapa ni kutoka maeneo mbalimbali ndani ya nchi na nje ya nchi huku hakiitaja baadhi ya mikoa kuwa wagonjwa kutoka mikoa hiyo wameweza kutibiwa.

Aliitaja baadhi ya mikoa kuwa ni Dodoma, Dar es salaam, Singida, Iringa na Songea na kueleza kuwa wagonjwa wote waliogundulika kuwa na tezi dume wamepatiwa matibabu na wote wamepona na hakuna aliyepoteza maisha.

Kutokana na hali hiyo Dk. Rugakingira alitoa wito kwa wanaume wote wenye umri kuazia miaka 45 kuhakikisha wanapima afya zao kwani ni rahisi kwa mwanaume kuwa na ugonjwa wa tezi dume.

Alisema kuwa ugonjwa wa tezi dume siyo ugonjwa wa ajabu kwani kila mwanaume analo tezi dume lakini kadri umri unavyosonga mbele na kuanzia miaka 45 kwa mwanaume anaweza kukumbwa na ugonjwa huo.

“Nipende kuwashauri wanaume wote kuanzia miaka 45 kwenda kliniki ili kuweza kupima ugonjwa wa tezi dume, kila mwanaume analo tezi dume ila kadri umri unavyokwenda na hasa kuanzia miaka 45 na kwenda mbele mwanaume yoyote anaweza kupatwa na ugonjwa huo wa tezi dume.

“Hata hivyo kwa sasa katika hospitali ya Benjamini Mkapa hupo utaalamu wa kutosha kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi katika kutibu tezi dume bila kufanya upasuaji kwani iko njia ya kuondoa tezi dume kwa kutumia njia ya ndani kwa ndani au kutibu kwa kutumia matundu badala ya kufanya upasuaji mkubwa unaoasababisha kuwepo na kidonda,” alieleza Daktari bingwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!