KIWANDA cha Iphone cha Zhengzhou, China kimetoa ahadi ya kuhakikisha usalama kwa wafanyakazi walioamua kuondoka na wale watakaobaki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kiwanda hicho kimefikia uamuzi huo siku chache baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa Uviko 19 ambapo wafanyakazi wa kiwanda hicho walionekana katika video zilizosambaa mtandaoni zikiwaonyesha wafanyakazi wakikimbia kutoka kwenye kiwanda hicho.
Menejimenti ya kiwanda hicho ilitoa notisi tatu siku ya Jumapili wiki iliyopita ikiahidi mpango wa mazingira salama kwa wafanyakazi wake.
Kiwanda hicho, kinachoendeshwa na kikundi cha Teknolojia cha Foxconn cha Taiwan na kinachodaiwa kuwa kituo kikubwa zaidi cha Iphone, kilikuwa kimeweka hatua kali za udhibiti wa ugonjwa huo kwa siku 10 zilizopita.
Sheria hizo zilijumuisha vipimo vya kila siku na marufuku ya kula kwenye kantini ya kiwanda hicho.
Leave a comment