JESHI la Polisi mkoani Kagera limetoa taarifa ya awali ya ajali ya Ndege ya Precision Air iliyotokea leo tarehe 6 Novemba, 2022 wilayani Bukoba mkoani Kagera na kusema ndege hiyo imeanguka ndani ya umbali unaokadiriwa kuwa mita 100 kutoka ulipo uwanja wa ndege Bukoba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Bukoba … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amekiri kutokea kwa ajali hiyo na kusisitiza zoezi la uokozi linaendelea hivyo watu wasikusanyike kuelekea kwenye eneo la ajali kwa sababu tayari kumejaa.
“Saa 2:35 leo asubuhi tulipokea taarifa ya ajali ya ndege ya Precision ikitokea Dar es salaam kuja Bukoba ndege ikiwa kama mita 100 ikapata taharuki kwa sababu maeneo yetu hali ya hewa ilikuwa mbaya, mvua ilikuwa inanyesha ikatumbukia kwenye maji.
“Kila kitu kipo under control Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama tunaendelea na uokoaji, naomba Wananchi wawe na subira wakati tunaendelea kuokoa,” amesema taarifa hiyo.
Leave a comment