Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kirigini kuzikwa leo Butiama
Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love

 

MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman Kirigini, unatarajiwa kuzikwa leo Jumamosi, kijijini kwao Muryaza, Wilaya ya Butiama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Kirigini alifarikini dunia tarehe 23 Mei 2023, baada ya kuanguka ghafla akitoka chumbani kwake katika nyumba yake iliyoko Musoma Mjini, mkoani Mara.

Jana Ijumaa tarehe 26 Mei 2025, mwili wa kirigini ulitolewa heshima za mwisho nyumbani kwake Musoma Mjini, kisha ulisafirishwa kuelekea Butiama kwa ajili ya mazishi.

Kufuatia msiba huo, Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ametoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu jamaa na marafiki, huku akichangia mahitaji mbalimbali kufanikisha mazishi.

Miongoni mwa michango hiyo ni, mchele kilo 100, maharage kilo 30, ssukari kilo 25, ngano kilo 25 na mafuta lita 20.

Mbali ya kuwa mbunge, Kirigini aliwahi kuwa Waziri wa Kilimo na Mifugo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!