Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba
Afya

Madaktari bingwa 10 waliokuwa India warudi na shuhuda nzito kuhusu utalii tiba

Spread the love

MADAKTARI bingwa wa upasuaji wa ubongo wameendelea kuongezeka katika Taasisi ya Mifupa (MOI) na kufikia 16 hali ambayo imeendelea kuifanya Tanzania kuwa kivutio cha utalii tiba Kusini mwa Jangwa la Sahara. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Madaktari hao walikuwa India kwa siku 10 wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii Tifa Taifa, ambaye ni Mkurugenzi wa Global Education Link na Global Medicare, Abdulmalik.

Mollel alipewa ruhusa na Mwenyekiti wake, Profresa Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, (MNH) kuongozana na ujumbe huo .

Hayo yalisemwa jana jijjini Dar es Salaam na daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mgongo wa taasisi hiyo, Nicephorus Rutabasibwa, wakati akizungumza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Terminal III.

Mkurugenzi wa Global Education Link na Global Medicare katikati Abdulmalik Mollel akiwaongoza madaktari bingwa wa Tanzania waliokuwa Inid akutembelea hospitali mbalimbali kwaaajili ya kuongeza thamani ya utalii tiba hapa nchini.

Alikuwa akizungumza wakati yeye na madaktari bingwa 10 waliporejea kutoka India ambapo walikwenda kutafuta fursa za kushirikiana na hospitali mbalimbali za nchini humo ikiwa ni jitihada za kukuza utalii tiba hapa nchini.

Alisema waliangalia nguvu ya Tanzania katika matibabu na kwamba hawakukuta tofauti sana kwani vifaa tiba na rasilimali watu ya madaktari iliyoko kule ni kama iliyoko hapa nchini.

“Wana vifaa vya kufanyia upasuaji ambavyo nasisi tunavyo, wanavifaa vya kufanyia uchunguzi kama MRI na ST SCAN ambavyo nasisi tunavyo kitu kipya ni matumizi ya roboti ambayo hawana hata miaka mitano nasisi tutajipanga kufikia huko. Tumeangalia fursa za kushirikiana nao katika kufundisha madaktari ,”  alisema

Aidha, serikali ya awamu ya sita imewekeza vifaa vya kisasa na rasilimali watu kwenye taasisi hiyo hivyo kuweza kumudu kufanya upasuaji wa teknolojia ya hali ya juu kama ilivyo India.

Makamu wa Rais wa Kampuni inayomiliki hospitali za YASHODA Group, Phanindra akizungumza na ujumbe wa madaktari bingwa kutoka nchini Tanzania ambao ulikuwa nchini India kwa siku 10 kutafuta fursa za kushirikiana kama njia ya kukuza utalii wa tiba hapa nchini.

“Waambieni watanzania na waafrika wengine kwamba mtu mwenye shida ya upasuaji wa ubongo au upasuaji wa aina yoyote wa mifupa halazimiki tena kwenda India anaweza kuja MOI mambo yakaenda vizuri kabisa na akaokoa gharama,” alisema

Kwa upande wake, taasisi ya saratani ya Oceanroad (ORCI), ilisema inauwezo wa kufanya utalii wa tiba Afrika kutokana na kuwa na vifaa tiba vya kisasa na madaktari bingwa wa kutosha kama ilivyo mataifa mengine kama India.

Daktari bingwa wa saratani wa taasisi hiyo, Dk Calorine Swai, ambaye ni daktari bingwa ya saratani Taasisi hiyo, aliyasema hayo aliporejea na ujumbe wa madaktari bingwa 10 kutoka Indiaa ambako walikwendaa kuangalia fursa.

Madaktari hao walikwenda India ambako walikaa kwa siku 10 wakiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utalii Tifa, Abdulmalik Molle, kuangalia namna ya kushirikiana na hospitali hizo katika utalii tiba.

Alisema kwa upande wa vifaa vya matibabu na madaktari bingwa aliowashuhudia nchini humo ni kama waliopo kwenye taasisi hiyo hivyo wana uhakika wagonjwa kutoka mataifa mengi Afrika wanaweza kuja ORCI na kupata tiba kamili.

“Tofauti ndogo niliyoona ni kuwa na viwanda vingi vya kutengeneza vifaa tiba na dawa za saratani na hali hiyo imeifanya huduma ya saratani kwao kuwa rahisi sana kupatikana kila inapohitajika. Tumeona mashine ya mionzi waliyonayo wenzetu imekwenda mbele kwa teknolojia  ya kisasa lakini tutafika,” alisema

Madaktari bingwa wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Utalii Tiba, Abdumalik Mollel wakiwa kwenye picha ya pamoja na wenzao wa India walipokwenda kwaajili ya utalii tiba

Alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa anaoendelea kuufanya kwenye sekta ya afya kwa ununuzi wa vifaa tiba na kuajiri wataalamu wabobezi kwamba ndio kunaifanya Tanzania kuanza kuwa kivutio cha utalii tiba Afrika.

Naye Mollel alisema ujumbe huo ulikuwa unatafuta wabia muhimu je ni nani katika wabia hawa yuko mamkini kufanya naye kazi katika uboreshaji wa huduma za afya zitakazovutia nchi jirani kuona Tanznaia kama kituo muhimu cha kupata tiba.

Molle pia alisema waliangalia fursa kwaajili ya kuwajengea uwezo wataalamu wa tiba Tanzania kwenye sekta ya afya na kwamba miongoni mwa mafanikio makubwa waliyopata ni kufika kwenye miji mikubwa mitatu nchini India ambayo imefanikiwa sana katika utalii tiba duniani.

“Tulianzia mji wa Hyderabad ambapo tulikaa siku nne tukaenda Bangarole na kisha tukahamia mji wa New Delhi na katika miji hiyo tumepitia hospitali nyingi na wadau wengi wa afya kujifunza kuhusu upatikanaji wagonjwa kutoka nje ya nchi, teknolojia zipi zitumike,” alisema Mollel na kuongeza

“Huwezi ukazungumzia utalii tiba bila kutaja hospitali kama Apollo ambao imeshafanyakazi hii kwa miaka zaidi ya 20, pia tulienda hospitali kama BLK, Fortis, Medanta, Yashoda, Rainbow ambayo ni maalum kwa watoto wadogo na HCG ambayo imebobea kwenye saratani,” alisema

Alisema hospitali ya Yashoda ni kundi la hospitali nne zenye jumla ya vitanda 4,000 wakati HCG ni kundi la hospitali 24, Rainbow kundi la hospitali kama  17 na mtandao wa Hospitali za Appolo wenye hospitali 70 na Fortis yenye hospitali 10 na vituo vya afya chini yake.

Alisema hospitali zote walizotembelea ndizo kwa kiwango kikubwa zimechangia mapinduzi makubwa kwenye utalii tiba nchini India kwa kushirikiana na serikali yao na kwamba ziliwapokea vizuri na kuunga mkono na kupongeza mtazamo wa serikali ya Tanzania kutaka kuipaisha kwenye huduma za afya duniani.

“Walitupokea vizuri na wakaipongeza Tanzania kwamba imekuwa na uhusiano mzuri sana na India na inatoa huduma kwa kushirikiana na mataifa mbalimabli ikiwemo India kwenye sekta ya afya na imekuwa kimbilio la watu wengi wakiwemo wawekezaji walisema ni nchi ya amani na kimbilio la watalii wa kawaida kwa hiyo hili ni jambo jema,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!