May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiongozi Yanga, aibukia Azam FC

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Azam Fc imemtambulisha katibu Mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga, Dk. Jonas Tiboroha kuwa mkurugenzi Mkuu wa mpira. Anaripoti Wiston Josia, Tudarco…(endelea)

Dk Tiboroha ametambulishwa hii leo jijini Dar es Salaam, Agosti 16, 2021. Kwenye ofisi za klabu hiyo Mzizima.

Kiongozi huyo alitambulishwa mbele ya wanahabari na mtendaji Mkuu wa timu hiyo Abdukarim Amin (Popat), kwa kumkabidhi rasmi nembo mpya ya klabu hiyo ambayo ataanza kitumikia.

Mara baada ya kutambulishwa Dk Tiboroha alisema kuwa moja ya sababu iliyomfanya kukubali wito huo ni mara baada ya kuona klabu hiyo inataka mafanikio.

“Moja ya sababu iliyonifanya mimi nikubali ni mara baada ya kuona nini Azam wanataka kufanikiwa.”

“Mimi naenda kutimiza malengo ya Azam Fc yaliyowekwa, ili uweze kufanikiwa kunavitu utakuwa umeviweka.” Alisema Tiboroha

Aidha kiongozi alitanabaisha majukumu yake na kueleza kuwa, kazi yake kubwa ni kusimamia maendeleo ya mpira ndani ya Azam FC, kwa timu za rika zote.

“Kazi yangu ni kusimamia shughuli zote za maendeleo ya mpira ndani ya klabu ya Azam kuanzia timu kubwa hadi za vijana pamoja na kuangalia ustawi mzima, ni zaidi ya utawala” alifunguka Tiboroha

Kiongozi huyo aliongezea kuwa wanakazi ya kufanya ndani ya klabu hiyo na kuomba ushirikiano ili kutimiza  malengo.

Alisema “Tuna kazi ya kufanya, ninacho kiomba kwako unipe ushirikiano, binafsi najua cha kufanya ili malengo tuliokubaliana kufikia yafikie.”

Ikumbukwe kabla ya kuibukia Azam FC Dk Tiboroha ambaye pia ni meneja wa mchezaji Simon Msuva, alishawahi kuhudumu ndani ya klabu ya Yanga kwenye nafasi ya ukatibu Mkuu kwa kipindi cha Miaka  miwili kuanzia 2014 mpaka 2016.

error: Content is protected !!