Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Naibu Waziri akagua anwani za makazi Shinyanga, atoa maagizo
Habari Mchanganyiko

Naibu Waziri akagua anwani za makazi Shinyanga, atoa maagizo

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew (mwenye kaunda suti) akikagua nguzo yenye jina la barabara na mtaa
Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew ameitaka Halmashauri ya Shinyanga kutenga fedha kutoka katika mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa kuweka miundombinu ya mfumo Anwani za Makazi na Postikodi. Anaripoti Patricia Kighono, TUDARCo … (endelea)

Mhandisi Mathew ametoa maagizo hayo juzi Jumamosi, tarehe 14 Agosti 2021 alipokagua miundombinu ya mfumo huo katika Manispaa ya Shinyanga.

Mpaka sasa utekelezaji uliofanyika kwa mujibu wa taarifa aliyopatiwa ni kusimika nguzo zenye majina ya barabara na mitaa kwenye Kata nne na mitaa 11 kati ya Kata 17 na mitaa 55 ya manispaa hiyo.

Alisema ili kutekeleza mfumo huo lazima fedha za mapato ya ndani zitengwe katika zoezi zima la kuipa majina mitaa na barabara kwa kushirikiana na wenyeviti wa mitaa husika ili majina yatakayopendekezwa na kuridhiwa ndio yaandikwe kwenye nguzo zinazoonesha majina ya barabara na mitaa ya eneo husika.

Mhandisi Kundo alisema Serikali imetenga kiasi cha Sh.1.1 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa Mfumo huo katika Manispaa ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Alisema kiasi hicho cha fedha kitatumika kuweka na kusimika nguzo zinazoonesha majina ya barabara na mitaa, kuweka namba za nyumba pamoja na zoezi zima la ukusanyaji wa taarifa za makazi, majengo na huduma zinazotolewa katika majengo hayo mfano hospitali, shule, benki.

Pia, majina ya barabara, mitaa, majengo na kuingiza taarifa hizo kwenye programu tumizi ya simu za mkononi ya NAPA

Mhandisi Kundo alisema taarifa zote zikiingizwa kwenye programu ya NAPA kwa usahihi zitasaidia na kumuwezesha mwananchi yeyote kufika mahali popote anapohitaji kufika iwapo akiwa na anwani kamili ya eneo hilo na kuiingiza kwenye programu tumizi ya simu za mkononi ya NAPA ambayo itamuonesha ramani na barabara ya kupita itakayomfikisha katika eneo husika analotaka kufika iwe nyumba ya mtu, hoteli, hospitali au sokoni

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko kwa nyakati tofauti wameishukuru Serikali kwa kutenga fedha za kutekeleza miradi ya mawasiliano Mkoani humo na kuahidi watahakikisha wanasimamia utelelezaji wa miradi hiyo ikiwemo mradi wa usimikaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwa ufanisi mkubwa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!