June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Upinzani washinda urais Zambia

Hakainde Hichilem

Spread the love

 

HAKAINDE Hichilem, Mgombea wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND) nchini Zambia, ametangazwa mshindi wa urais akimuangusha Edger Lungu, aliyekuwa akitetea nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tume ya Uchaguzi Zambia (ZEC) imemtangaza Haikande kuwa mshindi jana Jumapili usiku tarehe 15 Agosti 2021 kwa kupata kura 2,810,777 dhidi ya 1,814,201 alizopata Lungu.

Hichelim mwenye miaka 59 ameibuka mshindi wa nafasi hiyo baada ya kujitosa kugombea mara tano mwaka 2006, 2008, 2011 na mwaka 2016 ambazo zote alishindwa.

Mwanasiasa huyo wa upinzani anayejulikakana kama ‘HH’ ni mfanyabiashara wa kilimo na utalii mwenye shahada ya uchumi pamoja na shahada ya juu ya biashara aliyoipata Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza.

Edger Lungu

Chama cha Patriotic Front kiliingia madarakani mwaka 2011 chini ya uongozi wa Michael Sata na mwaka 2015, Edger Lungu alichaguliwa baada ya kifo cha Sata aliyekuwa madarakani.

Katika harakati zake za kuwania kuingia Ikulu, tarehe 11 Aprili 2017, Hichilema alijikuta matatizoni baada ya Jeshi la Polisi nchinbi humo kumkamata akiwa katika makazi yake na kufunguliwa mashtaka ya kusaliti nchi.

Rais huyo mteule, katika mahojiano aliyofanyiwa kwenye kipindi cha Hardtalk alisema, akiwe mahabusu alikaa siku nane pasina kupewa chakula, maji, mwanga na kumpulizia maji ya pilipili akituhumiwa kutaka kumuua Rais Lungu.

Alisema, mke wake Mutinta, alikuwa akifika kumpeleka chakula lakini hakuruhusiwa kuonana naye.

error: Content is protected !!