Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kigogo CUF, wenzake wafutiwa kesi ya uhujumu uchumi
Habari za Siasa

Kigogo CUF, wenzake wafutiwa kesi ya uhujumu uchumi

Mhandisi Mohammed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari -CUF
Spread the love

 

MKURUGENZI wa Habari, Uenezi, Mahusiano na Umma wa Chama cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania, Mhandisi Mohamed Ngulangwa na wenzake watano, wamefutiwa kesi ya uhujumu uchumi, iliyokuwa inawakabili katika Mahakama Kuu Iringa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi Na. 6 iliyofunguliwa na Serikali mwaka 2018, imefutwa leo Jumanne, tarehe 12 Oktoba 2021, mbele ya hakimu aliyepewa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, Hakimu Mkazi, Respicius Mwaijage.

Kesi hiyo ilifutwa mbele ya mahakama hiyo, baada ya upande wa Jamhuri kuieleza kwamba haina nia ya kuendelea nayo na kuomba ifutwe.

Awali, kesi hiyo ilidumu kwa miaka mitatu bila kusikilizwa na au upelelezi wake kukamilika.

Mbali na Mhandisi Ngulangwa, wengine waliokuwa wameshtakiwa kwa kesi hiyo ni, Mhandisi Godwin Mshana, ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Ujenzi ya MNM Engineering Service Limited. Prof. Philemon Mushi, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Mkwawa kuanzia 2007 hadi 2012.

Wengine ni, Prof. John Machiwa, aliyekuwa Makamu Mkuu wa chuo hicho, kitengo cha utawala (2009-2012) na Jackson Matandu, Mjumbe wa Bodi ya Zabuni.

Ngulangwa ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa Habari CUF, alidaiwa kutenda kosa hilo akiwa Meneja Miliki na Mjumbe wa Bodi ya Zabuni ya Chuo Kikuu cha Mkwawa.

Ngulangwa na wenzake walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 2018, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia hasara Serikali ya Sh. 2.4 bilioni, alizolipwa mkandarasi MNM Engineering Service Limited, katika mradi wa ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa.

Hata hivyo, Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ya ukaguzi maalum ya 2018, ilibainisha kwamba hakuna Fedha iliyopotea kwenye mradi huo na kwamba mkandarasi huyo alikuwa amelipwa pungufu ya fedha aliyostahili kulipwa, mpaka aliposimamishwa kazi Julai 2017.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!